Na
Bashir Yakub
Makala
zilizopita nilieleza mambo au taarifa muhimu zinazopaswa kuwa kwenye mkataba wako
unapokuwa unanunua
nyumba/kiwanja. Nikasema katika
niliyosema kuwa mkataba lazima uoneshe ukitokea mgogoro utatatuliwa vipi, ueleze kuwa
utapotokea mgogoro muuzaji lazima
awajibike kuhakikisha anakupa ushirikiano mnunuzi
ili kumaliza mgogoro huo na kuwa
muuzaji kama ana mke
basi mke wake ni lazima aandaiiwe
nyaraka iitwayo ridhaa ya
mwanandoa ambayo ni tofauti
na mkataba na aisaini
pamoja na kuweka picha yake.
Nilieleza mengi lakini hayo ni baadhi tu. Kwa wale ambao hawakubahatika kuyasoma hayo basi waandike neno MAKALA SHERIA kwenye google watapata makala hizo. Leo
tena naeleza hatua muhimu sana au
ya lazima na lazima haswaa kwa mnunuzi wa kiwanja/nyumba ambayo anatakiwa apitie
kabla ya kufanya manunuzi.Hatua hii kwa
jina la kitaalam huitwa
OFFICIAL SEARCH kwa lugha rahisi tu waweza kuiita utafiti,upekuzi, upembuzi au upelelezi rasmi ambayo hufanywa na wanasheria. Mi napenda
niite upelelezi.
( 1 ) AINA
ZA VIWANJA/NYUMBA UNAPOTAKA
KUFANYA UPELELEZI KUJUA
KAMA KUNA MGOGORO.
Nyumba/viwanja tunavyouziana kila siku
vimegawanyika katika hadhi
mbalimbali. Kwanza kuna
nyumba/viwanja vyenye hati, vyenye
leseni za makazi, vyenye ofa na ambavyo havina hati, leseni ya makazi wala ofa.
Kutokana na makuzi ya miji yetu viwanja/nyumba zenye hati mara nyingi huwa ni chache sana.Zenye leseni
za makazi ni nyingi kiasi na haya ni maeneo ambayo hasa hujulikana kama uswahilini. Zenye ofa huwa
ni chache nazo kwakuwa ofa ni
hatua anayopitia mtu anapoelekea kupata hati au leseni ya makazi. Pia
maeneo ambayo hayana hati wala leseni ya
makazi wala ofa nayo ni mengi sana
pia. Kwa Dar es salaam haya ni maeneo ya pembeni pembeni
mwa mji Tegete,bunju, pugu, chanika, mbagala, baadhi ya maeneo ya kigamboni n.k. Hata hivyo eneo liwe na hati leseni ya makazi au hapana
bado kisheria linatambulika .
( 2 )
NAMNA YA KUJUA
KAMA NYUMBA/KIWANJA KINA
MGOGORO
Kama
kiwanja/nyumba ina hati kuna maombi
rasmi ya kisheria ambayo huwa yanafanywa kwenda ardhi
wizarani, wizara ya ardhi makao
makuu kwa Dar es salaam na kwa mikoani maombi hayo
mara nyingi huenda makao makuu ya
mkoa ambapo katika maombi hayo
mnunuzi anaiomba mamlaka ya ardhi imjulishe mambo yafuatayo;
( a ) KUJUA JINA
LA MMILIKI HALALI
WA NYUMBA/KIWANJA.
Kwanza
kujua jina la mmiliki. Jina hili
linatakiwa kufanana sawasawa bila
tofauti yoyote na yule mtu
anayetaka kukuuzia eneo. Hii husaidia
kuthibitisha kuwa anayeuza ndiye kweli mmiliki wa eneo.Kama
majina yatatofautiana basi haraka sana
achana na hilo eneo ili kuepuka mgogoro.
( b ) KUJUA KAMA NYUMBA/KIWANJA
UNACHONUNUA KIMEWEKWA KAMA DHAMANA
YA MKOPO.
Kitu kingine unachouliza kwenye hayo maombi rasmi
ni kama hiyo nyumba/kiwanja
kimewekwa kama dhamana kwa ajili ya vitu kama mkopo . Wakati mwingine
yawezekana mtu kukuuzia eneo ambalo
limewekwa dhamana kwa mkopo wa hela nyingi tu. Na kisheria kama
eneo limewekwa dhamana yule anayelimiliki
kwa dhamana ndiye mwenye nalo kwa
muda huo na wewe uliyenunua sheria iko wazi unakuwa umeliwa. Ieleweke kuwa ni vigumu sana kujua kama eneo unalouziwa limewekwa dhamana au hapana ikiwa hukufanya upelelezi huu. Wakati mwingine mtu huweka dhamana eneo lake na
kubaki na hati . Kwa hati ile
wewe mnunuzi ni rahisi
kuhadaika kuwa eneo ni lake lakini kumbe ni eneo lenye deni kubwa. Ukinunua eneo kama hilo utakuwa
umenunua mgogoro mkubwa ambao wewe mnunuzi kushindwa na kunyanganywa
ulichonunua ni lazima tu.
( c ) KUJUA KAMA KUNA MGOGORO WA
KIFAMILIA.
Kitu
kingine ambacho utaomba kujua katika
yale maombi ni kama
kuna mgogoro wowote wa
kifamilia kama migogoro ya
mirathi, migogoro ya kindoa ambapo
mwanandoa mmoja anaweza kuwa ameweka
zuio kuhusu uuzwaji wowote wa
nyumba/kiwanja hicho. Usipofanya upelelezi huu utanunua halafu siku ya
kubadilisha jina ndio siku utajua kuwa eneo lile lilikuwa haliruhusiwi kuuzwa.
Aidha
ifahamike kuwa mamlaka za ardhi hupata taarifa hizi za viwanja vya watu kupitia
utaratibu wa mazuio uitwao CAVEAT.
( 3 ) MNUNUZI WA
ENEO LENYE LESENI YA MAKAZ I
AKAFANYE UPELELEZI WAPI.
Maeneo
yenye leseni za makazi
maombi haya ya upelelezi wa
kiwanja/nyumba yanapelekwa manispaa.
Manispaa inayohusika ni ile
ambayo lilipo eneo husika . Kwa
mfano ukitaka kununua eneo
kinondoni manispaa ya kinondoni ndiyo
inayopelekewa maombi, kama eneo
unalotaka kununua lipo temeke basi manispaa ya temeke ndio
ipelekewe maombi. Aidha
kuhusu mpangilio wa maombi
na kile unachotaka kujua kuhusu
eneo ni kama nilivyoeleza hapo juu kwenye
hati .
( 4 ) MAENEO AMBAYO HAYANA HATI,
LESENI ZA MAKAZI
UPELELEZI HUFANYIKAJE.
Kwakuwa
maeneo ya namna hii yanakuwa hayana nyaraka
yoyote maalum katika mamlaka za
serikali basi wakati mwngine huleta ugumu
kidogo katika kujua ukweli ili kuepuka mgogoro. Lakini kitu ambacho huwa tunashauri katika
maeneo ya hivi ni kuwa kwanza muuzaji akueleze eneo alilipataje. Kama
alilinunua kwa mtu ni vema akaonesha ule
mkataba alionunulia na kama mauzo
yatafanyika basi ni lazima mnunuzi apate
kopi ya ule mkataba. Pili kama amelirithi ni lazima aoneshe fomu ya usimamizi wa mirathi ambayo ndiyo itakuwa inampa mamlaka ya kuuza. Na kama alipewa zawadi basi aonesha
waraka wa zawadi ( deed of
gift) ambao umesajiliwa.
Jingine la msingi sana katika
maeneo yasiyo na hati wala
leseni za makazi huwa
ni kuuliza majirani. Eneo unalonunua kama wapo majirani hebu waulize
tu kwa nia njema na mara nyingi ukiwapata wawili watatu hivi ni rahisi kupata ukweli au
kukuwezesha kujenga shaka. Na majirani usiwaulize kwa pamoja, mtafute mmoja
mmoja kila mtu kwa muda wake ili kuepusha kuoneana haya katika kusema ukweli.
Pia hakikisha wakati wa kuwahoji majirani muuzaji
asiwepo, we tafuta tu muda
wako nenda peke yako na pata taarifa. Uwepo wa muuzaji unaweza
kuingilia( influence) ukweli. Usikurupuke
utalia, ni hayo kwa leo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
No comments:
Post a Comment