Mkurugenzi wa Klabu hiyo .Domician Genad akitoa maelezo namna kambi hiyo inavyoendeshwa. |
Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini Dixon Busagaga akifanya mahojiano na mkimbiajiwa kimataifa wa mbio ndefu Osward Levelian anayejiandaa na mbio za Marathoni nchini China. |
Baadhi ya wakimbiaji wa kike wakiwa kambini Holili. |
Mwalimu wa timu ya riadha ya Holili,Timoth Kamili(mwenye t-shirt nyeusi )akizungumza na mkurugenzi wa klabu hiyo,Domician Genand. |
Na Dixon
Busagaga,Moshi.
BAADA ya Tanzania kuendelea kufanya vibaya katika mbio za kimataifa za
Kilimanjaro Marathoni klabu ya Riadha ya Holili (HYAC) ya mkoani
Kilimanjaro imelazimika kuwapeleka wanariadha wake watatu nchini Kenya
kwa ajili ya mazoezi ya mbio ndefu za Kilometa 42 .
Hatua hiyo imekuja baada ya wakimbiaji kutoka nchini Kenya kuendelea
kuwaburuza wanariadha wa kitanzania katika mbio hizo ambazo hufanyika
kila mwaka na kushirikisha mataifa zaidi ya 40 huku
zikishirikisha
wakimbiaji zaidi ya 6000.
Akizungumza na Globu ya Jamii mkurugenzi wa Holili Youth Athletics
Club ,Domician Genand alisema wanariadha hao ambao wanatarajia kurudi
nchini Kesho walienda nchini humo kwa ajili ya kupata uzoefu toka kwa
wanariadha wanao shiriki mbio mbalimbali za kimataifa.
“Ninao wanariadha watatu ambao niliamua kuwapeleka nchini Kenya kwa
ajili ya kutusaidia ili wafanye mazoezi ya kilometa 42 kutokana na
uwepo wa makocha wazuri na wazoefu katika mbio hizo”alisema
Genand.
Alisema mbali na wanariadha hao pia wapo wanariadha wengine kutoka
katika klabu yake ambao wamekuwa katika mazoezi Mbulu mkoani Arusha na
wengine watakao shiriki mbio fupi za Kilometa 21 na kilometa tano wao
wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika maeneo ya Holili.
Genand alisema klabu yake bado imekuwa na Changamoto mbalimbali licha
ya kwamba baadhi ya wafadhili wamejitokeza angalau kupunguza baadhi ya
mahitaji kwa wanariadha hao wanaotarajia kushiriki mbio za
Kilimanjaro
Marathoni.
“Unapokuwa unaweka mtu kambini kuna mahitaji mengi sana anayokuwa
anahitaji,sisi tulijaribu kuandika andiko ambalo linaweza kutubeba
katika kipindi hiki cha Kilimanjaro Marathoni na tulikuwa na bajeti ya
Sh Mil,5 wapo ambao wametusaidia kama Marenga Investment,Bonite
Bottlers na John Hudson muandaaji wa mbio za Kilimanjaro”alisema
Genand.
Mbio hizo zinadhaniwa kuwa kati ya mbio kubwa zaidi duniani za kitalii
na ndio tukio kubwa zaidi la kimichezo Tanzania. Kilimanjaro Marathon
ya mwaka huu inatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 6,000
wakiwemo
takribani wageni 800 kutoka nchi zaidi ya 40.
Mbio za Kilimanjaro Marathon 2015 zinaratibiwa na Executive Solutions
kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Riadha Kilimanjaro na Kilimanjaro
Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager,
Tigo,
GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, CMC
Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA,
NSSF, Bodi ya Kahawa Tanzania, na Kilimanjaro Water.
No comments:
Post a Comment