Moja ya Jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya mtaa wa Libya na Mosque likiendelea kuwaka moto huku Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiangalia namna ya kuudhibiti moto huo.
Gari la Zimamoto la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam likiwasili eneo la tukio.
Kazi ikiendelea.
Mara mabomba kadhaa yakazidiwa na nguvu ya maji na kupasuka,lakini haikuwa tatizo kwani ilikuwe mingine kibao ya rizevu.
Kazi ikiendelea.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akijaribu kufanya mawasiliano na vyombo mbali mbali vya zimamoto.
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio la Moto Mkubwa uliozuka mapema leo kwenye majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yaliopo kwenye makutano ya mtaa wa Libya na Mosque kuteketeza eneo lote la juu la Majengo hayo.Chanzo cha moto huo hakikuweza fahamika mpaka tunaingia mitamboni japo tetesi zinaeneleza kwamba ni hitilafu ya uemem.
Kazi zilisimama kwa watu wengine wa maeneo ya jirani na tukio hilo.
Vikosi vya Zimamoto toka makampuni mbali mbali vilijipanga vyema kabisa kukabiliana na tukio hilo.
Kikosi cha Zimamoto cha Faya kikiendeleza uhodari wake wa kuzima moto ulioenea kila pembe ya majengo hayo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Jeswad Nkongo akizungumza na vyombo vya habari juu ya walivyofanikiwa kuudhibiti moto huo.
Mwanalibeneke Othman Michuzi (kushoto) akiwa katika mavazi maalum pamoja na Maafisa wa Kikosi Zimamoto wakati wa zoezi la uzimaji moto huo mchana wa leo jijini Dar.
Sasa tumemaliza kazi na shukrani za dhati kwa maafisa wa kikosi cha Zimamoto waliokuwa bega kwa bega na wanahabari kuhakikisha uzimaji wa moto huo unakwenda vema.
No comments:
Post a Comment