Sunday, February 22, 2015

BALOZI SEIF IDDI MGENI RASMI KWENYE MAHAFALI YA SHUO CHA ELIMU YA BIASHARA PEMBA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi tuzo na fedha taslim kijana Mohammed Suleiman Khalfan baada ya kuwa Mwanafunzi Bora wa Fani ya Hesabu katika chuo cha Elimu ya Biashara Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akimzawadia Tuzo na Fedha Taslim Mwanafunzi Bora wa Fani ya Mawasiliano ya Umma wa Chuo cha Elimu ya Biashara Pemba Nassor Mussa Khamis kwenye mahafali ya chuo hicho hapo Vitongoji Chake Chake Pemba.
Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Baishara Pemba wakiandamana kuingia katika uwanja wa Michezo wa Chuo cha Amali Vitongoji kwa ajili ya Hamafali yao baada ya kumaliza mafdunzo yao ngazi ya Cheti.
Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Pemba wakiwa tayari kuthibitishwa kukamilisha mafunzo yao na kupewa vyeti vyao kwenye mahafali yao ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Pemba wakifuatilia matukio mbali mbali kwenye mahafali yao iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Amali Vitongoji Chake chake Pemba.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Bodi ya chuo cha elimu ya Baishara pamoja na Serikali Mkoa wa Kusini pemba mara baada ya kukamilika kwa mahafali ya kwanza ya chuo hicho.Kulia ya Balozi Seif ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo akiwa pia Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Nd. Hemed Suleiman Abdullah, Mkuu wa Chuo hicho Abdulwahab Said Abubakari na Mhadhiri wa chuo hicho Moh’d Said. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuja Majid na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Bibi Hanuna Ibrahim Masoud.
Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na Uongozi na wahadhiri wa chuo cha elimu ya Biashara Pemba mara baada ya kukamilika kwa mahafali ya kwanza ya chuo hicho tokea kilipoanzishwa Januari 2014. Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments: