Pc Damiani Christiani wa polisi mkoa wa Singida,akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati wa zoezi la kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
PC.Abdalah Ramadhani kutoka trafiki makao makuu Dar-es-salaam,akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati zoezi la kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mrakibu msaidizi wa Jeshi la polisi (ACP) mkuu wa kitengo cha elimu kwa umma makao makuu ya usalama barabarani jijini Dar-es-salaam,Abel Swai,akiwahamasisha abiria wa basi la kampuni ya France line lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Arusha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo watagundua dereva mlevi au akiendesha gari vibaya,ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya"Wait to send"inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
MRAKIBU msaidizi wa polisi makao makuu kitengo cha elimu kwa umma usalama barabarani (trafiki) ACP,Abel Swai,amewataka madereva wa mabasi nchini, kuhakikisha wanakuwa watanashati kwa kuvaa nguo zinazolingana na unyeti wa kazi yao,ili waweze kujijengea mazingira mazuri ya kukubalika na kuaminika na wateja wao (abiria.
ACP Swai metoa wito huo jana wakati akisimamia zoezi la kupima ulevi madereva wa mabasi na kuhakikisha sheria,taratibu na kanuni za usalama barabarani kama zinatekelezwa ipasavyo.Zoezi hilo linaloendeshwa na Jeshi la polisi kwa ushirikiano na Baraza la Taifa la usalama barabarani na Vodacom Tanzania,lilifanyika katika kituo kikuu cha mabasi mjini Singida.
Alisema kwamba wapo baadhi ya madereva wa mabasi licha ya kutofaa sare ya kampuni zao akiwa barabarani,wanavaa nguo ambazo hazifafani na heshima ya kazi anayoifanya, kitendo ambacho baadhi ya abiria kupunguza imani kwake kwa kudhani sio dereva makini.
"Kazi ya udereva wa mabasi ina heshima ya kipekee.Kwa hiyo ni lazima dereva pamoja na kutekeleza kazi yake kikamilifu,pia anapaswa awe nadhifu kwa mavazi yake na vitendo vyake vingi vikubalike mbele ya jamii",alifafanua zaidi ACP Swai.
Kuhusu zoezi lao,mratibu huyo msaidizi,alisema sambamba na zoezi la kudumu la kupima madereva walevi,pia wamekuwa wakikangua madereva watumiaji wa vyombo vya moto,watembea kwa miguu na wasukuma matoroli kama wanazingatia kikamilifu sheria zote za usalama barabarani bila shuruti.
"Lengo letu ni kuwakumbusha madereva,abiria na wananchi kwa ujumla wajibu wao wawapo barabarani.Abiria kama wanagundua gari wanalosafiria ni mbovu,wamecheleweshwa,dereva ni mlezi au makosa yo yote ya jinai,atoe taarifa haraka kwa jeshi la polisi.Hali kadhalika madereva watimize wajibu wao kwa mujibu wa sheria.Wakati wote wazingatie au waheshimu alama na mistari iliyowekwa barabarani"alisema.
Alisema endapo kila Mtanzania atatambua anatakiwa afanye nini ili kuokoa maisha ya mwezake,ajali ya barabarani zinazopotesha maisha ya watu na mali zao,zitapungua kwa kiasi mkikubwa.
ACP Swai ametumia fursa hiyo kuwakumbusha madereva kuacha kutumia pombe wakati wakiwa barabarani kwa madai kwamba zinasabaisha wakose umakini na kunza kutoa maamuzi ambayo ni hatari kwao na wateja wao.Pia amesema ni marufuku mabasi ya masafa marefu kuwa na dereva mmoja,ni lazima wawe wawili.
Katika zoezi la kupima madereva watumiaji wa pombe wakiwa barabarani, lililofanyika mjini hapa jana,madereva wawili wa nje ya mkoa huu,waligundulika kutumia pombe na wanashikiliwa na jeshi la polisi mjini hapa.
No comments:
Post a Comment