Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla amefanya ziara ya vijiji mbalimbali Mbeya Vijijini ambako amezindua mradi mkubwa maji vijiji vya Shongo na Igale maelfu wafurahia. Katika ziara hiyo kaagiza wakala wa visima (DDCA) kuchimba kisima kirefu kijjiji cha Mjele kutekeleza ahadi ya mhe Rais Jakaya Kikwete kuwaokoa wananchi maelfu kufuata maji umbali wa kilomita 7. Pia ametoa ahadi ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maji wa maji vijiji vya Iwindi,Mwashiwawala na Izumbwe ambao ulisimama baada mkandarasi kusimamishwa kwa kushindwa kazi.
Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akikwepa utelezi wakati akikagua chanzo cha maji ya chemchemu ya Ndoba kijiji cha Galijembe
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akipokea zawadi kijiji
cha Shongo
ambapo wananchi walimlaki kwa furaha
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla katika Akipanda mti
chanzo cha Ndoba- kijiji cha Galijembe
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akizindua rasmi mradi kijiji cha Shongo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla apokelewa kwa
shangwe kijiji cha shongo
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akizindua Maji kijiji
cha shongo
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla na mbunge wa Mbeya Vijijini mch Luckson Mwanjale (kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi mradi maji
kijiji cha shongo
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akiwa na machifu kijiji cha Shongo
No comments:
Post a Comment