Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali,
akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayotumika kuonyesha aina za
mizigo inayopakiwa kwenye ndege wakati wataalam hao walipotembelea Kampuni hiyo,
mwishoni mwa wiki kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali,
akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, ngazi mbalimbali zinazotumika wakati
abiria wanaposhuka kutoka kwenye ndege, wakati wataalam hao waliotembelea Kampuni hiyo.
Moja ya magari yanayomilkiwa na kampuni ya kuhudumia mizigo, ndege na
abiria ya Swissport, likitumika kuitoa ndege na kuiweka kwenye Barabara ya kiungio (tax way)
kabla haijaondoka, kama lilivyokutwa mwishoni mwa wiki.
Moja ya magari yanayomilikiwa na Kampuni ya kuhudumia ndege, abiria na Mizigo
ya Swissport, yanayotumika kushusha mizigo kutoka kwenye ndege, kama lilivyokutwa
mwishoni mwa wiki wakati wataalam kutoka Wizara ya uchkuzi, walipotembelea kampuni hiyo
kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa ndege mbalimbali zinazotua
katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
Ndege za mashirika mbalimbali zinazofanya safari zake kutoka Tanzania kwenda Nchi za nje, zikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Idadi ya abiria wanaowasili na kuondoka katika viwanja vya ndege nchini imeendelea kuongezeka kutoka abiria 2,172, 519 mwaka 2005 hadi abiria 4,670,380 mwaka 2013, sawa na ongezeko la asilimia 14.8. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment