Saturday, January 10, 2015

TATIZO LA KUTOAMINIANA LITAATHIRI UTEKELEZAJI WA SDGs- –TANZANIA

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason akiwa pamoja na baadhi ya washiriki wa majadiliano hayo kushoto kwake ni Balozi Tuvako Manongi anaonekana pia Balozi wa Finland mwenye Tai nyekundu Bw. Kai Sauer
Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akizungumza wakati wa majadiliano baina ya wajumbe wa Bodi ya Global Impact ambayo ni Taasisi ya Umoja wa Mataifa na Wawakilishi wa Balozi mbalimbali na kumshirikisha pia Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw, Jan Elliason.
Bw. Paul Polman CEO wa Unilever akizugumza wakati wa majadiliano hayo ambapo katika maelezo yake, alitambua juhudi za Serikali ya Tanzania za kujenga mazingira yanayoziwezesha sekta binafsi kukua na kuchangia maendeleo ya nchi.
Sehemu wa washiriki wa majadiliano hayo yaliyoambata na chakula cha mchana, majadiliano hayo yaliandaliwa kwa pamoja baina na Wakilishi za Kudumu za Tanzania, Finland na Bagladesh.
Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla akiwa na washiriki wengine wa majadiliano hayo kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika utekelezaji wa ajenda mpya za maendeleo endelevu na mchango wa serikali katika kuziwezesha sekta hizo kutekeleza majukumu hayo.

Na Mwandishi Maalum,   New York

Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania  imesisitiza  kwamba,  ili utekelezaji wa  malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 uwe wenye tija, Jumuiya ya Kimataifa inapashwa  kulitafutia ufumbuzi tatizo la kuto kuaminiana baina ya serikali na wafanyabiashara.

 Hayo yameelezwa  mwishoni mwa wiki na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,   Balozi Tuvako Manongi  wakati wa   mkutano wa majadiliano wa Wajumbe wa Bodi ya  Taasisi ya  Umoja wa Mataifa ijulikanayo kama Global Compact waliokutana hapa Umoja wa Mataifa kwa  Mkutano wao kwanza wa Bodi hiyo kwa mwaka huu.

Katika  majadiliano hayo  ambayo pia yalihudhuliwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Bw. Jan Elliason, Wajumbe wa Bodi na wawakilishi wengine zaidi ya  30 yaliandaliwa kwa pamoja baina ya Wakilishi za Kudumu za Tanzania, Finland na Bangladesh.

Balozi Manongi amesema   kuna  tatizo kubwa la kutoaminiana baina ya serikali na wafanyabiashara jambo analosema  kama halitashughulikiwa   linaweza kuathiri utekelezaji wa SDGs, utekelezaji ambao unahitaji sana ushirikiano na uhusiano kati ya  sekta binafsi, serikali na wadau wengine.

Wakati wa majadiliano hayo wajumbe walibadilishana mawazo kuhusu wajibu na nafasi ya  sekta binafsi katika utekelezaji wa  ajenda  mpya za maendeleo baada ya 2015. Aidha walijadiliana  kuhusu nafasi ya serikali katika kutoa motisha kwa  sekta binafsi   ili kwayo ziweze kushirikiana na serikali  katika utekelezaji wa ajenda hizo za maendeleo.

Amesema  msingi wa kiini cha mafanikio ya  ushirikiano kati ya serikali na wafanyabiashara katika utekelezaji wa  ajenda za maendeleo endelevu lipo suala la namna gani  bora ya kushughulikia suala la   kuaminiana miongoni mwa wadau.

Na kuongeza kuwa litakuwa jambo la muhimu sana kushughulikia sula hilo la upungufu wa kuaminiana miongoni mwa wadau na kwamba Taasisi hiyo ya Global  Impact inayofursa nzuri na mchango wa mkubwa wa kutoa katika kujenga  kuaminiana na  kujiamini.

Akizungumzia   juhudi za serikali  katika  utekelezaji wa  sera ya  ushirikiano  na uhusiano kati ya serikali na sekta binafsi (PPP)  na hasa kuelekea utekelezaji wa  ajenda mpya za maendeleo, Balozi amewaeleza washiriki hao kuwa Tanzania siyo tu inatambua na kuthamini ushirikiano huo bali pia  imjitahidia sana  katika  uboreshaji wa mazingira yanayoziwezesha sekta binafsi kutekeleza majukumu yake  licha ya kukiri kwamba bado kuna mapungufu ya hapa na pale.


Akasema Tanzania inatambua kwamba serikali na wafanyabiashara wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga mifumo, sera na taratibu shirikishi zitakazotoa motisha kwa  watendaji wa sekta binafasi kutoa mchago katika ukuaji wa uchumi endelevuvu na ujenzi wa viwanda ili kutoa ajira.

No comments: