Friday, January 16, 2015

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA SANAA,UBUNIFU NA UTAMADUNI NCHINI OMAN

Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman kushoto akimsikiliza Mkuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshirikia Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman Bi Khadija Batash, katikati ni Afisa wa Ubalozi Bw. Abdallah kilima.
Mbunifu na mchongaji wa Milango maarufu kama “Zanzibar Door” Bw. Abdul-Rahman akipaka rangi baadhi ya kazi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman kulia akibadilishana mawazo na mmmoja ya Wajasiriamali kutoka Tanzania anayeshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.
Salum ameir Muchi Mchoraji akiwaonesha baadhi ya kazi zake Wageni waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.
Mbunifu na Mchongaji “Big Mama” akionesha kazi zake Wageni waliotembelea katika Banda la Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.

Shamra shamra za ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.
Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Oman Dkt. Fuad bin Jaafar al Sajwan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonesho ya Mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman. Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanziabr
Jumla ya Wajasiriamali 20 kutoka Tanzania, Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.

Taasisi hizo ni pamoja na Kamisheni ya Utamaduni Zanzibar, Baraza la Sanaa Zanzibar, Hoteli ya Bwawani, Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Omani.

Maonesho hayo ambayo yatadumu kwa muda wa Mwezi mmoja yamefunguliwa usiku wa Jana na Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Oman Dkt. Fuad bin Jaafar al Sajwan.

Akizungumzia Maoneosho hayo Naibu Balozi wa Tanzania nchini humo Juma Othman amesema Maonesho yana leongo la kuzikutanisha nchi Rafiki za Omani kutangaza Vipaji vyao na  fursa za kimaendeleo zinazopatikana katika nchi husika.

Amesema ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kuitumia katika kutangaza vivutio vyake, Vipaji vyake na Utamaduni wake jambo ambalo kama litatumika vyema linaweza kuipandisha hadhi zaidi Tanzania.

“Kwa ujumla tumejiandaa na nawaomba Wageni na wenye asili ya Tanzania kuja katika Banda letu kujionea mambo mbali mbali na bidhaa zinazotengenezwa na vipaji vya watu wetu” Alisema Naibu Balozi.

Bwa Othman amesema Nchi ya Omani imekuwa na kawaida ya kufanya Tamasha hilo na kualika nchi Rafiki ambapo China, India, Iran na Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki Tamasha hilo litakalochukua muda wa mwezi mmoja.

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo kutoka Tanzania Bi Khadija Batash amesema Watahakikisha kuwa wanazitangaza vyema Fursa za kimaendeleo  zinazopatikana Bara na Zanzibar ili kuifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusonga mbele kimaendeleo.

Amesema Tanzania imejaaliwa Raslimali nyingi ikiwemo Mbuga za Wanyama, Fukwe nzuri za Zanzibar na utamaduni wa kipekee na kwamba kama utatangzawa vyema Sekta ya Utalii itapiga hatua zaidi ya kimaendeleo.

Ameongeza kuwa Vipaji vya ubunifu wa Kuchora, Kuchonga na kufuma vinaweza kuwasaidia sana Watanzania na kuitangaza vyema kimataifa iwapo Wabunifu hao watawezeshwa vyema na Serikali au taasisi binafsi.

Aidha amewataka Washiriki kuzidisha Mashirikiano miongoni mwao ili kuiletea Sifa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Maonesho hayo ya muda wa mwezi mmoja yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10 za jioni na kufungwa saa 04 usiku kwa majira ya nchi ya Omani.

No comments: