Monday, January 5, 2015

RAIS KIKWETE AMWAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI IKULU DAR LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini nyaraka wakati wa hafla fupi ya kumwapisha, George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi nyaraka za Serikali, George Mcheche, baada ya kumwapisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kutoka kulia) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makindajaji Mkuu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othuman, Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche, aliyeteuliwa, wakiwa katia ukumbi wakisubiri zoezi hilo la kuapishwa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akisubiri kuapishwa, George Mcheche, akizungumza jambo na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, wakati wa hafl hiyo.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na viongozi wa ngazi za juu.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wakuu wa Ulinzi na usalama.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wanafamilia wa Bw. George.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wenzake.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi Tume ya Sheria.Picha na OMR.

1 comment:

Anonymous said...

Hivi Ikulu imeshindwa kuwatoa watu wanao zagaa zagaa huko nyuma wakati picha za matukio kama haya zinachukuliwa?