Tuesday, January 20, 2015

NGO's YA APEC KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI DODOMA YAFUNGA MAFUZO KWA WAENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MKOANI HUMO

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akiongea katika kufunga mafuzo kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Muwakilishi wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Dodoma, Bw. Erasto Kasugu akisoma risala kwa mgeni rasmi,wakati wa kufunga mafuzo kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi..
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la APEC  Bw. Respicius Timanywa akiongea jambo kwenye ufungaji wa mafunzo hayo
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akikabidhiwa zawadi na waendesha pikipiki(Bodaboda).
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akikabidhi vyeti vya mafunzo kwa washiriki.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi toka Jeshi la Polisi.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa shirika la APEC.

Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP David Misime amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wengine litaendeleza msako kwa wale wote waendesha pikipiki ambao hawana leseni kwani walishapewa muda mrefu ili waweze kupata leseni pamoja na mafunzo ya udereva.


Ameyasema hayo wakati wa kufunga mafuzo kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,mafunzo yaliyochukua wiki moja kuanzia tarehe 12/01/2015 hadi tarehe 19/01/2015.


Kamanda Misime amesema elimu waliyoipata waendesha pikipiki (bodaboda) waitumie vizuri ili kujiepusha na ajali ambazo kwa kiwango kikubwa zinasababishwa na makosa ya kibinadamu na ukosefu wa mafunzo.


Aidha Kamanda Misime ameeleza kuwa takwimu za kuanzia mwezi Januari hadi Desemba 2014 zinaonyesha ajali za pikipiki zilifikia 62, kati ya hizo ajali za vifo ni 16 ambazo zilisababisha vifo vya watu 18. Pia ajali za majeruhi zilikua 28 na jumla ya watu 31 walipata majeraha sehemumbalimbali.


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Ant – Poverty and Development Care (APEC) Bw. Respicius Timanywa amesema kutokaa na ajali za barabarani kuwa nyingi hapa nchini, imebainika kuwa ajali nyingi za vifo na majeruhi ni za waendesha pikipiki wasio na mafunzo stahiki na utafiti uliofanywa na APEC kwa Mkoa wa Dodoma, umebaini kuwa waendesha pikipiki wengi kutokuwa na elimu ya usalama barabarani, leseni za udereva na kutokuwepo na mahusiano mazuri kati yao na Jeshi la Polisi jambo linalosababisha ongezeko la ajali za barabarani na vurugu.


Pia amezitaja changamoto mbalimbali zilizopo katika kazi ya APEC ni muitikio mdogo wa walengwa ambao ni madereva wa vyombo vya moto, madereva wenye leseni bila vyeti vya kutoshiriki mafunzo katika vyuo mbalimbali.


Akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu wa waendesha pikipiki (Bodaboda) Manispaa ya Dodoma Bw. Erasto Kasugu  amesema katika mafuzo haya waendesha pikipiki wapatao 193 kutoka maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Dodoma wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani na pia walieleza changamoto zinazowakabili ambazo ni kukabwa na kuibiwa pikipiki, madereva wa magari makubwa hususani malori kutowathamini waendesha pikipiki wanapokuwa barabarani, baadhi ya abilia kukataa kuvaa helmet, baadhi ya waendesha pikipiki kuvaa jina la bodaboda huku wakifanya vitendo vya uhalifu pamoja na baadhi ya waendesha pikipiki kukataa kushiriki mafunzo ya usalama barabarani kama yaliyotolewa na APEC.


Aidha wamesema kwa kuwa wamepata mafunzo ya Polisi Jamii na mbinu za kuwakamata waalifu, wameomba ushirikiano mkubwa pindi wanapotoa taarifa za matukio yasiyofaa baada ya kuwatilia shaka au kuwabaini waarifu.

No comments: