Thursday, January 15, 2015

MHE. CHIKU GALLAWA AZINDUA MSIMU WA KILIMO KWA MWAKA 2015 KATIKA MKOA WA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa alipowasili kijijini hapo Januari 13,2015 kuzindua msimu wa kilimo Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaelezea wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa malengo ya kuzindua msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaelekeza wakina mama wa kijiji cha Damai Kondoa namna bora ya kupanda kwa nafasi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaonesha kwa vitedo wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa namna bora ya kupanda mazao kwa mstari na nafasi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa wakshiriki zoezi la kupanda mahindi kwa mstari na nafasi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mhe. Chiku Gallawa pamoja na baadhi ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma wakiwaonesha kwa vitedo wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa namna bora ya kupanda mazao kwa mstari na nafasi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mhe. Chiku Gallawa akiteta jambo na vijana Ramadhani Ismail (kushoto) na Shafii Ayoub wa kijiji cha Damai Kondoa waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma wale wenye tabia ya kuombaomba chakula cha msaada kuachana na tabia hiyo mara moja kwani ni aibu kwa kaya zenye tabia hiyo, wilaya na Mkoa  kwa ujumla ukizingatia fursa za kuzalisha chakula cha kutosha kujikimu mwaka mzima na kuzalisha ziada kwa ajili ya kujiongezea kipato ipo.

Ili kufanikisha azma hiyo Mhe. Chiku Gallawa amewataka wananchi wa Dodoma kuendesha shughuli za kilimo kwa kufuata kanuni za kilimo bora ikiwa ni pamoja na kuandaa mashamba mapema, kutifua mashamba, kuwahi kupada mwanzoni mwa msimu wa mvua, kupanda kwa nafasi inayostahili, kuzingatia matumizi ya mbegu bora, matumizi ya mbolea za viwandani au za wamyama, kufaya palizi na kulima kwa kuweka makinga maji maneo ya miteremko ama milima.

Hayo ameyasema mwanzoni mwa wiki (Januari 13, 2015) Wilayani Kondoa alipokuwa akizindua msimu wa kilimo kwa mwaka 2015 katika Mkoa wa Dodoma ambapo aliwataka wananchi kutambua msimu wa kilimo umeanza wananchi wajikite kwenye kufanya kilimo bora, pia watumie taarifa za utabiri wa  hali ya hewa kujua hali ya upatikanaji wa mvua.

Mhe. Gallawa akiwa ameambatana na baadhi ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma, viongozi wa Halmashauri zote za wilaya Mkoa wa Dodoma wataalamu wa kilimo kutoka wilaya zote Mkoani humo walitumia zoezi hilo la uzinduzi wa msimu wa kilimo kuwaonesha kwa vitendo wanachi wa kijiji cha Damai Kondoa namna bora ya kulima kwa kufuata kanuni za kilimo bora kama kutumia mbolea, kupanda kwa nafasi na matumizi ya mbegu bora.

Mhe Gallawa alitumia nafasi hiyo pia kuwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya za Dodoma kuhakikisha kwenye kila kijiji kunakuwa na Daftari la Kilimo na Mifugo ambalo litakua linatunza taarifa muhimu za shughuli za kilimo na mifugo zinazofanywa na wananchi vijijini na kutaka wataalam kilimo na mifugo kuyasimamia kwa umakini. Vlevile alikemea vikali tabia ya wataalam kujazana ofisini badala ya kutoka kwenda vijijini kwa wananchi kutoa huduma za kitaalamu.

Akijibu hoja ya changamoto ya soko la mazao wanayozalisha wananchi wa Dodoma Mhe. Gallawa amewataka wataalamu wa serikali ya Mkoa na Wilaya wa masuala ya biashara, Kilimo, ushirika na masoko wawe wanakaa mapema kabla ya msimu wa kilimo kuanza ili watafute masoko ikiwezekana hata utaratibu wa kilimo cha mkataba na kuwaelekeza wakulima mazao ya kulima kabla hata ya msimu.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge alibainisha kuwa zoezi hilo la uzinduzi wa Msimu wa Kilimo Kimkoa limeshafanyika kwa miaka mitatu mfululizo kweye wilaya za Kongwa, Chamwno na Bahi na malengo yake ni kuhamasisha wananchi kanuni za kilimo bora.

Mshauri wa kilimo mkoa wa Dodoma Bw. Bernard Abraham  ameelezea kilimo katika mkoa wa Dodoma kuwa kinaumhimu wapekee kwani asilimia 75% hadi 80% ya wakazi wa Dodoma ni wakulima wakati ukienda maeneo ya vijiji vya Dodoma karibu wakazi wake wote wanategemea kilimo kuendesha maisha yao. Mbali na mkakati huo wa kufanya uzinduzi Rasmi wa Kilimo, ameahidi yeye na wataalamu wenzie wa kilimo wataendelea kubuni mikakati zaidi ya kunyanyua kilimo Mkoani Dodoma.

No comments: