Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Vuai Ali Vuai kuelekea kukishiriki upandaji wa mboga
mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na
nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya
washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.
Kinana
amemaliza ziara ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar ambapo
amekagua na kushiriki ujenzi katika miradi 40 mikoa 12.
Katika ziara hiyo,Ndugu Kinana alijionea mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofanywa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, zikiwemo barabara,
hospitali, elimu na maji pamoja na kusambazwa umeme karibu kila kona.
Katika
ziara hiyo ,Ndugu Kinana amewataka viongozi wa dini na Serikali kukemea kitendo
cha CUF kuwaita wanaohamia CCM makafiri. Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alimpongeza Ndugu Kinana kwa ziara yake, kwamba
imekuwa ya mafanikio makubwa na imewapa somo na moyo wa kuimarisha chama
visiwani.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji wa mboga
mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na
nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya
washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kushiriki upandaji wa Mboga mboga na
kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la
ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika
wapatao 15.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM-Kusini
Pemba,Bakari Mshindo akielekea kushiriki upandaji wa Migomba katika
shamba la Ushirika la Utandawazi Cooperative Society katika kijiji cha
Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji Migomba katika
shamba la Ushirika la Utandawazi Cooperative Society katika kijiji cha
Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Kwa mujibu wa
taarifa iliyosomwa na mmoja wa viongozi wa Ushirika huo alieleza mbele
ya Kinana kuwa Ushirika huo una jumla ya watu 25,na wanajishughulisha na
ufugaji wa Kuku wa Kienyeji,Mboga mboga pamoja na Migomba katika shamba lenye ekari mbili na nusu.
Komredi Kinana akiwa na
baadhi ya viongozi wengine wa chama na serikali wakiomba dua walipozuru
kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Hayati Dk. Omari Ali Juma eneo la
Wawi Digilini, Wilaya ya Chakechake, Pemba.
Copy and WIN : hhttp://bit.ly/copynwin
Copy and WIN : hhttp://bit.ly/copynwin
Komredi Kinana akiwa na
baadhi ya viongozi wengine wa chama na serikali wakiomba dua walipozuru
kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Hayati Dk. Omari Ali Juma eneo la
Wawi Digilini, Wilaya ya Chakechake, Pemba.
Copy and WIN : hhttp://bit.ly/copynwin
Copy and WIN : hhttp://bit.ly/copynwin
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya Wilaya mara baada ya kusomewa na kukabidhiwa taarifa
fupi ya uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Wilaya na Mkoani.
Pichani
ni moja ya Jengo la tawi ya ofisi ya CCM Milimuni ambapo katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Kinana alishiriki ujenzi wake,katika jimbo la Chambani,wilaya
ya Mkoani Kusini Pemba.
Balozi
wa shina namba moja ,Balozi Ame Vuai Shein akisoma taarifa yake mbele
ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,alipokwenda kumtembelea katika kijiji
cha Kadarani Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,kusini
Pemba.
Baadhi ya wananchi na wafuasi
wa chama cha CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara.
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),alipokuwa akihutubia jioni leo.
Baadhi ya wananchi na wafuasi
wa chama cha CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza mbele ya Wananchi na wafuasi wa
chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa
mpira wa Mjimbini,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Ndugu Kinana
amehitimisha ziara yake ya siku 15 ndani ya Kisiwa cha Unguja na Pemba
jioni ya leo,
ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment