Thursday, January 8, 2015

Jubilee Insurance kutumia M-PESA kuwawezesha mamilioni ya watanzania wenye kipato cha chini kujiunga na bima ya Afya

Naibu kamishina wa Bima Tanzania, Juma Makame (katikati) akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee Insurance, George Alande (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa wakati akisaini nyaraka za makubaliano ya huduma ya BimaAFYA kati ya Vodacom Tanzania na Jubilee Insurance itakayotolewa kupitia huduma ya M PESA, ambapo Watanzania wenye kipato cha chini watajiunga na huduma hiyo na kupata matibabu kwenye hospitali zaidi ya 150 nchini. Ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga namba *150*57#. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya BimaAFYA kati ya Vodacom Tanzania na Jubilee Insurance itakayotolewa kupitia huduma ya M PESA, ambapo watanzania wenye kipato cha chini watajiunga na huduma hiyo na kupata matibabu kwenye hospitali zaidi ya 150 nchini. Ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga namba *150*57#. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee Insurance, George Alande na Naibu Kamishina wa Bima Tanzania, Juma Makame. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa huduma ya BimaAFYA kati ya Vodacom Tanzania na Jubilee Insurance itakayotolewa kupitia huduma ya M-PESA, ambapo Watanzania wenye kipato cha chini watajiunga na huduma hiyo na kupata matibabu kwenye hospitali zaidi ya 150 nchini. Ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga namba *150*57#.
Naibu Kamishina wa Bima Tanzania, Juma Makame (katikati) akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee Insurance, George Alande (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzani,a Kelvin Twissa wakipongezana baada ya uzinduzi wa huduma ya BimaAFYA kati ya kampuni zao itakayotolewa kupitia huduma ya M-PESA, ambapo Watanzania wenye kipato cha chini watajiunga na huduma hiyo na kupata matibabu kwenye hospitali zaidi ya 150 nchini .Ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga namba *150*57#. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Kamishina wa Bima Tanzania, Juma Makame (kulia) akioneshwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa jinsi ya kujiunga na huduma ya BimaAFYA wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kati ya Vodacom na Jubilee Insurance itakayowanufaisha wananchi wenye kipato cha chini kupata matibabu kwenye hospitali zaidi ya 150. Huduma hiyo itapatikana kupitia huduma ya M-PESA ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga namba *150*57#. Anaeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee Insurance, George Alande.

Hatimaye sekta ya bima nchini imerahisisha huduma za bima ya afya kwa kuwawezesha watanzania wenye kipato cha chini kujiunga na huduma mpya ya  bima ya afya iliyozinduliwa na kampuni ya Jubilee Insurance Tanzania itakayotelwa kupitia huduma ya M-PESA.

Huduma hii mpya ya BimaAfya ina unafuu mkubwa na inawalenga watu binafsi na familia kwa ujumla na inamuwezesha atakayejiunga na huduma hii kupata huduma za matibabu katika hospitali zaidi ya 150 nchi nzima –wenye magonjwa ya kutibiwa mara moja,wagonjwa wenye magonjwa yanayopelekea walazwe hospitalini na akina mama wajawazito watakaojiunga na huduma hii watatibiwa bure!
Uchangiaji wa kujiunga katika mfumo wa BimaAfya umerahisishwa ili kuwawezesha wananchi kujiunga kulingana na vipato vyao,upo uchangiaji wa mwezi,mara tatu kwa mwezi,nusu mwaka na mwaka mzima.

“Tanzania kama zilivyo nchi nyingine za Afrika kwa muda mrefu haina utamaduni unaowawezesha wananchi wake wote kuchangia na kufaidika na mfumo wa bima ya afya zaidi ya wafanyakazi ambao wameajiriwa katika sekta rasmi na hali hii inatokana na gharama za kuchangia bima ya afya kuwa kubwa kiasi cha kuwashinda wenye vipato vya chini kuzimudu ambapo kuna idadi kubwa ya watanzania wameachwa nje ya mfumo huu muhimu ambao ni muhimu kila mtu kujiunga nao.BimaAfya itawawezesha watanzania kujiunga nayo kama ambavyo wanapata huduma za kifedha kupitia huduma ya M-PESA” Anasema Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelivin Twissa.
                                                                              
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa kampuni ya  huduma za bima ya Jubilee George Alande,amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 18 ya watanzania ndio wanafaidika na huduma za bima ya afya nchini wengi wao wakiwa ni waajiriwa.Kuna watu wachache wasio kwenye ajira ambao wanaweza kulipia viwango vya bima za afya vilivyopo hivi sasa-hali inayopelekea wananchi wengi waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi kuachwa nje ya mfumo huu wakiwemo wakulima,madereva wa daladala na wengineo wengi.

Pia takwimu kutoka Mamlaka ya Usimamizaji wa Huduma za Bima nchini (TIRA) za mwaka 2013 zinaonyesha kuwa  waliokata bima  za afya nchini ni asilimia 19% ya bima zote zilizokatwa.Hali hii inaonyesha kuwa kupitia huduma ya BimaAfya iliyozinduliwa leo inapaswa kuchangamkiwa na watanzania wote hususani wale wenye vipato vya chini.Ubunifu wa huduma hii kwa kiasi kikubwa utawezesha kila mtanzania kupata huduma za bima kwa urahisi kutoka kwa kampuni inayoongoza katika kutoa huduma za bima Afrika Mashariki.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Edge Point ambayo pia ina ubia katika ushirikiano huu wa kutoa huduma ya BimaAfya,Lilian Makoi amesema kuwa matumizi  ya teknolojia ni  njia pekee ya kurahisisha huduma za kifedha kwa watanzania wote wanaoishi mijini na vijijini na wenye vipato vya aina mbalimbali ambao hapo awali ilikuwa ni vigumu kwao kupata huduma za kifedha kama vile kujiunga na huduma za bima ya afya.


“BimaAfya imebuniwa kuwapunguzia mzigo wa gharama za matibabu watanzania wenye kipato cha chini hususani wale waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi.Huduma hii itawawezesha kupata huduma za matibabu katika hospitali zaidi ya 150 nchini bila kulipa fedha taslimu.Malengo yetu ya baadaye ni kusambaza huduma hii nchi nzima ili kuwawezesha wananchi wengi kuchangia na kunufaika” alisema Ms Makoi.

Kujiunga na huduma hii  ya BimaAfya anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom ni kupiga simu namba *150*57# na kutoa taarifa za awali zinazotakiwa.Kinachofuatia ni  kuchagua jinsi ya kufanya malipo kwa kadri ya uwezo wake kupia huduma ya M-Pesa.Baada ya hapo atapata namba ya utambulisho ya BimaAfya ambayo atakuwa anaitumia pindi atakapohitaji kupata huduma kutoka hospitali zilizosajiliwa kutoa huduma hiyo.Kujiunga na huduma hii ni kuanzia umri wa miaka 18 pia watoto wadogo wa wateja waliojiunga watafaidika na huduma hii.Vigezo na masharti ya kujiunga yanaelezwa  wakati wa mchakato wa kujiunga.

No comments: