Thursday, January 22, 2015

BALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN AKUTANA NA WATANZANIA WANAOSHIRIKI MAONESHO YA SANAA NA UTAMADUNI MJINI MASCUT

Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akisalimiana na Mwandishi wa Chanel Ten Said Makala Ofisini kwake alipowaita kwa lengo la kuwapa nasaha Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman.
Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima kushoto akimkaribisha Balozi wa Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia kutoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Katikati ni Mkuu wa Msafara wa Watanzania hao Bi Khadija Batashy.
Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman,kushoto kwake ni Naibu Balozi wake Bw.Juma Othman.
Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
Mkuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika mjini Mascut, nchini Oman Bi Khadija Batashy akitoa shukran zake kwa niaba ya wenzake baada ya kupewa nasaha na Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh wa katikati, kulia kwake ni Naibu Balozi Bw.Juma Othman.
Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Wakuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman kulia ni Masha Hussein na kushoto ni Khadija Batashy.
Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni  yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman mara baada ya kuwapa nasaha zake. Picha zote na Faki Mjaka-Muscut Oman.

No comments: