Mfanyabiashara na mmiliki wa duka
la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth mshana akiongea na
Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma ya kufanya malipo
kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field Communication (NFC) based
solution ya Airtel Money. kadi hii maalum inamuwezesha mteja kufanya
malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa maalum tu mara moja, kisha
kuweka nambari ya siri na kufanya malipo mahali popote. kwa sasa huduma
hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Huduma hii ya Near Field
Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha kadi na kifaa tu kupitia
huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na
kampuni ya simu za mkoni ya airtel
Mama elizabeth mshana mmiliki wa
duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa kupitia kadi huduma iliyozinduliwa
na Airtel mkoani Arusha inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa
haraka zaidi kwa kutumia kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye
teknolojia ya Near Field Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa
na Airtel Money.akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde.
Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha
kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za
mkoni ya airtel.
Afisa uhusiano wa kampuni ya simu
za mkononi ya AIRTEL Jane Matinde akimuelekeza Moja ya wateja bi Merry
Ngowi jinsi ya kutumia kifaa na kadi maalumu ambacho hutumika
kukamilisha miamala ya malipo katika maduka mbalimbali. Huduma hii
ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya
mitandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya
airtel, tukio lifanyika mwishoni mwa wiki mkoani arusha eneo la muromboo
wakati wa uzinduzi huduma hiyo ambayo inaleta njia salama, ya haraka na
rahisi kwa wateja kufanya malipo.
Mfanyabiashara wa duka la chakula
katika eneo la Mrombo Arusha Bwana Elibariki Ngowi akipokea malipo
kutoka kwa mteja kwa kupitia kadi maalum ya Near Field Communication
(NFC) ya Airtel Money. , huduma imezinduliwa na Airtel mkoani Arusha
inawawezesha wateja wake kufanya malipo kwa kutumia kadi hiyo maalumu
kwa haraka bila huanza kupiga *150*60# hii unagusisha tu na kulipa
haraka kati kanti ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akishudia
huduma hiyo inavyofanya kazi. Huduma hii ya Near Field Communication
(NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza
kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.
……………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo (mwishoni mwa wiki) imetangaza huduma ya kwanza sokoni
inayotumia kadi maalumu kwa kupitia huduma ya Airtel Money. Huduma hiyo
mpya inayowawezesha wateja wa Airtel Money kufanya malipo kwa kutumia
kadi imeanza katika mkoa wa Arusha na itaendelea kufikishwa katika
mikoa mbalimbali nchini.
Akiongea kuhusu huduma hiyo,
Mkurugenzi wa Airtel Money Aijaza Khan alisema” technologia inakuwa kwa
kasi na tumeonelea ni muhimu kwenda sambamba na mabadiliko hayo kwa
kuleta huduma za kibunifu zitakazokithi mahitaji ya wateja wetu
yanayokuwa kwa kasi kila siku. Nia yetu ni kuona wateja wetu wanapata
huduma za kisasa kwa wakati wote.
Huduma hii mpya tunayoitambulisha leo
itawawezesha wauzaji na wanunuzi kupata njia rahisi, ya uhakika na
salama ya kufanya miamala na malipo yao ya kila siku. ili kutumia
huduma hii kila mteja atatakiwa kupata kadi maalum inayomuwezesha
kufanya malipo kirahisi , kwa haraka na kwa usalama katika maduka
mbalimbali yaliyopatiwa vifaa maalumu kwaajili ya kupokea malipo toka
kwa wateja. Huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wafanyabiashara na
wateja wetu Arusha.
“Kadi hii maalumu imeunganishwa na
akaunti ya Airtel Money ya mteja, mteja anachotakiwa ni
kugusisha kadi yake na kifaa cha kupokea malipo (POS) ili
kuweza kufanya malipo. Malipo yatakamilika pale mteja
atakapothibitisha muamala kwa kuweka namba yake ya siri kwenye
kifaa cha malipo.
Tunajivunia kuwa mtandao wa kwanza
Tanzania kuanzisha huduma hii ya kibunifu itakayowawezesha wateja wetu
kufanya malipo ya kwa urahisi, haraka , kiusalama bila kuwa na haja ya
kupiga namba ya Airtel money na kuingia kwenye orodha, Kwa kutumia kadi
maalumu mteja anaweza sasa kufanya malipo. ”. aliongeza Khan.
Akiongea kuhusu faida za huduma
hiyo , Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” huduma hii
inafaida nyingi kwa wafanyabishara na wateja ikiwa ni pamoja na njia
salama ya kuifadhi pesa, ya kuhakiki na kukusanya pesa,mfanyabiashara
anaweza kuzipeleka moja kwa moja benki kutoka kwenye kifaa hicho au
kutoa pesa kwa wakala aliye karibu. Kwa upande wa wateja faida hizo ni
pamoja na kufurahia urahisi, usalama, uharaka wa kufanya malipo na
pia kuepusha wateja kutembea na pesa nyingi mfukoni ili kufanya
malipo. Mteja atakapopoteza au kuibiwa kadi yake pesa zake kwenye kadi
yake zinabaki salama aliongeza” Matinde.
Akiongelea kuhusu uzoefu alioupata
a kutumia huduma hii ya kadi kupitia Airtel Money, Mfanyabiashara na
milliki wa Phamarcy Bi Elizabeth Mshana alisema” Huduma hii ni ya
kipekee na imerahisisha sana namna ya kufanya biashara maana ni rahisi
kutumia na ni salama. Wateja wanapokuja dukani kununua dawa na hawana
pesa taslimu mfukoni wanatumia huduma hii na mimi kama muuzaji nafurahi
kwakuwa pesa zangu ziko salama na sina haja ya kufikiri kuhusu kutafuta
chenji.
Kwa kweli ni huduma nzuri na tunaifurahia na nawashauri
wafanyabiashara wenzangu na wateja kutumia huduma hii kwani inaleta
ufanisi” Huduma hii inapatikana sehemu
mbalimbali ikiwemo maduka ya biadhaa , maduka ya chakula, maduka ya
dawa, mawakala wa Airtel Money na Baa, Mpango mkakati ni kufikisha
huduma hii katika maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu.
Airtel kupitia huduma yake ya
Airtel Money hivi karibuni imezindua huduma nyingine ya kibunifu
ijulikanayo kama Timiza inayowawezesha wateja wake kupata mikopo
rahisi papokwa papo na kurejesha baada ya wiki moja au mwenzi huduma
ambayo imewawezesha watanzania wengi kuboresha mitaji ya biashara zao na
kutatua changamoto ndogondogo za kila siku
No comments:
Post a Comment