Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5 bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars.Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel,Anethy Muga.
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5 bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wanne waliongia hatua ya 5 bora katika mashindano ya kuvumbua vipaji vya muziki ya Airtel Trace Music Strars . fainali za mashindano hayo zinategemea kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa pili.kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza washiriki walioingia tano bora katika shindano la Airtel Trace Music star,shindano lenye lengo la kusaka na kuibua vibaji kwa wanamuziki chipukizi.
Akiongea na waandishi wa habari,Meneja Masoko wa Airtel,Aneth Muga alisema" leo tunayofuraha kubwa kutangaza majina ya washiriki waliofanya vizuri katika mashindano haya na kupata nafasi ya kuingia katika hatua ya tano bora na kuweza kumpata mmoja kati yao atakaeibuka na ushindi wa kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Afrika".
Akiendelea kufafanua Aneth alisema "Washiriki hawa watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5), sasa kura nyingi toka kwa watanzania ndio itakayomuwezesha mmoja wao kupata ushindi wa kwanza wa Airtel Trace Tanzania.
Mashindano haya yanalengo la kuinua vibaji vya muziki kwa vijana wetu kuzifikia ndoto zao na kuwawezesha kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi. Airtel tunajisikia furaha kuwa sehemu ya mafanikio yao na sehemu ya kuinua vipaji vya wanamuziki chipukizi kwa kupitia mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars. Napenda kuwapongeza na kuwatia hamasa wale wote walioshiriki na pia hawa waliofanya vizuri na kufika katika hatua hii muhimu ya mashindano haya.
Akitangaza majina ya walioibuka kwenye tano bora Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema " tunawashukuru watanzania na wanamuziki chipukizi kwa kushiriki katika shindano hili na mpaka sasa tunao vijana wengi waliojaribu kuonyesha uwezo wao wa kuimba, lakini kama mnavyofahamu haya ni mashindao hivyo napenda kuwaleta kwenu wale waliofanya vizuri zaidi na kuingia katika hatua hii ya mchuano mkali.
waliobahatika kuingia tano bora ni pamoja na Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (YUN), Christopher Kihwele (TOJ), Tracy Eminence (MHR), Beautus Henry (BOB) na Rose Mbuya (ROS)
Natoa wito kwa watanzania , wadau mbalimbali na wapenzi wa muziki kuwapigia kura washiriki hawa kwa kupiga kutuma sms yenye jina la fumbo la mshiriki kwenda kwenye namba 15594
Hii ni nafasi ya pekee kwa watanzania kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika anga za Afrika hivyo ni matumaini yetu kuwa washiriki hawa watajifua vyema ili kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika pindi mshindi atakapo patikana.
Akiongea mara baada ya kutangaza kuwa moja ya tano bora Christopher Kiwhele alisema" najisikia furaha sana kupata nafasi hii ya kuwa moja ya tano bora, kwakweli kwangu ni kama ndoto, siamini kama nimeweza kufudhu ma kufika katika hatua hii kubwa, na amini ntaendelea kufanya vizuri kwani naendelea kujiandaa vyema, nimetamani sana kuwa mwimbaji nyota na mwimbaji anayenivutia zaidi ni Ed sheeran naamini kupitia mashindano haya ntafika mbali na kutumiza ndoto zangu. Nawaomba watanzania watuunge mkono na kutupigia kura ili kuendelea kufanya vizuri na hatimae kuwakilisha nchi yetu vyema katika mashindano ya Afrika.
Washiriki tano bora wa Airtel Trace music Star sasa wako kambini ambapo wanapata mafunzo yatakayoendelea hadi fainali inayotegeme kufanyika tarehe 7 mwenzi wa pili 2015 jijini Dar es saalam.
1 comment:
Nakutakia kila raheli my sister Rose Mbuya, Due to the fact umefika hapo, Mungu na azidi kukung'arisha. Be Blessed succeed in Jesus name.
Post a Comment