Naibu
Waziri wa Maji,Mh Amos Makala kulia akiwa anasikiliza maelezo kutoka
kwa Eng wa maji Bw.Mohamed Ismail katika eneo la chanzo cha maji mto
nduruma katikati niKaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga
Muonekano wa maporomoko ya maji mto nduruma ni chanzo kikubwa kinachotegemewa Mkoani Arusha katika huduma ya maji
Askari anayelinda eneo hilo
Na Pamela Mollel wa jamiiblog.
Naibu
Waziri wa Maji,Mh Amos Makala amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha
kuendelea kuwafichua wale wote wanaoshiriki katika wizi wa maji ili
waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.Alitoa
wito huo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa
lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya
upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa
maji
Waziri Makala alisema kuwa serikali inafanya jitihada ya kuboresha huduma ya maji ikiwa nipamoja na kuboresha miundombinu,kukomesha wizi wa maji kwa kutoa elimu kwa wananchi.“Wizi wa kujiunganishia maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini upo lakini kwa sasa tunaoparesheni ya kuwasaka wale wote wanaotumia maji bila kulipa watambue kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria”alisema Makala
Aidha katika moja ya chanzo kikubwa cha maji mto nduruma alisema kuwa chanzo hicho kinategemewa kwa mkoa wa Arusha hivyo alitoa pongezi kwa mamlaka ya maji kwa kuwa wabunifu.Naye Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga alisema kuwa kwa hivi karibuni walikuwa na zoezi la ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kufanikiwa kuwakamata watu wanaohujumu mamlaka hiyo takribani 750 hivyo zoezi hilo bado ni endelevu
No comments:
Post a Comment