Tunu Jamal (17) hivi sasa anasoma kozi ya kutimiza ndoto yake ya kuwa Ofisa Ugavi katika Chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology na ameanzia ngazi ya cheti ili akifanya vizuri aweze kujiendeleza zaidi.
Mbali na kozi hiyo anaungana na wenzake wanne wanaolelewa pamoja katika kituo cha Mwandaliwa kusoma kozi ya ushonaji ili ndoto yake isipotimia awe na ujuzi mbadala wa kuendesha biashara ya ushonaji.
“Nachukua mafunzo ya ushonaji wa nguo ili nisipofanikiwa katika fani ya ndoto yangu au nisipopata kazi haraka inayohusiana na kazi ninayoisomea niwe na kazi nyingine itakayoniwezesha kujipatia kipato cha kuendesha maisha yangu na kuweza kujitegemea”Anasema Tunu.
Kituo cha Kulea watoto yatima na wenye mazingira magumu cha Mwandaliwa mwaka huu kilipata msaada wa mashine za kushona nguo kutoka taasisi ya Vodacom Foundation ili kuwezesha kituo hicho kujitegemea badala ya kuendeshwa kwa kutegemea misaada.Darasa la ushonaji la kituo hicho hivi sasa lina cherahani ambazo zinawawezesha wanafunzi kujifunza fani ya ushonaji nguo.
“Tumeona mpango wa Mwandaliwa kujiendesha na tumetoa msaada utakaobadilisha maisha wanaolelewa katika kituo hiki,tumeona tuanze kusaidia mradi wa kufundisha watoto ushonaji kwa kuwa ni rahisi kutekelezwa na una uhakika wa kuwapatia kipato cha kuendesha maisha yao wakishapata ujuzi wa kutosha”.Anasema Reenu Verma,Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation na kuongeza kuwa lengo kuu na kusaidia mradi huu ni kuona kituo cha Mwandaliwa kinapata uwezo wa kujiendesha.
Lengo la kituo kuanzisha mradi wa ushonaji ni kupata fedha za kulisha watoto,pia watoto kwa upande wao wameonekana kuufurahia mradi huu unaowawezesha kupata ujuzi utakaowawezesha kujitegemea siku za usoni na kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa hivi yenye ushindani mkubwa.
Msimamizi wa kituo hicho Omar Kyaruzi ameishukuru taasisi ya Vodaom Foundation kwa kufadhili mradi huu wa ushonaji na kuongeza kuwa kwa muda mfupi umeonekana kuleta mafanikio kwa kuwa watoto wengi wamepata ujuzi na kituo kimeanza kupokea kazi za ushonaji wa sare za shule zilizopo jirani na kituo.
“Kupitia uwezeshwaji kama huu uliofanywa na taasisi ya Vodacom Foundation tumeanza kupata mafanikio ya kuelekea katika kujitegemea na tutaendelea kubuni miradi mbalimbali ya kusaidia kituo na watoto tunaowalea.Hivi sasa tuko mbioni kuanzisha kozi za kingereza,hesabu na mbinu za biashara ili kuwawezesha watoto kupata ujuzi utakaowawezesha kutimiza ndoto zao”.Anasema Kyaruzi.
Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya kuwawezesha wasichana ijulikanayo kama Girl Pawa inaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya kuwajengea uwezo wasichana na wanawake ili waweze kutimiza ndoto zao.
No comments:
Post a Comment