Thursday, December 4, 2014

WANACHUO WAWILI WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) DODOMA WAPATA GPA YA 4.9

Bw. Peragius  Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata  GPA 4.91 akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
Bi. May Issa  mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi  na kupata  GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.

Kwa kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanafunzi hawa  kutoka kampasi ya Dodoma  wameweza kupata ufaulu mkubwa katika masomo yao.

 Bi. May Issa  Mwanafunzi  aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa  Manunuzi  katika mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014 ametangazwa  kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata GPA ya  4.92. ambapo  aliweza kupata alama  A  28 , alama  B+ tatu  na  alama  B  moja  kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na  Bw. Peragius Cosmas  aliyepata GPA ya 4.91.

 Kwa upande  wake Mwanafunzi mwingine  Bw, Peragius Cosmas  aliye kuwa akisoma Shahada ya kwanza ya Uhasibu   yeye pia alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA ya  4.91  ambapo aliweza kupata alama  A  29 na  alama  B+ tatu    kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  uhasibu.

Hivi  karibuni katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)  pia tulishuhudia  Msichana   Doreen Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa  Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano.




 Bi. May  Issa akionekana mwenye furaha siku ya mahafali  ya 49 iliyofanyika hivi karibuni katika chuo cha Elimu ya biashara kampasi  ya Dodoma.
Bw. Peragius Cosmas akionekamna mwenye furaha  katika mahafali ya  49 ya  chuo cha CBE iliyofanyika hivi karibuni katika  Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dodoma.
  Rais mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi CBE  kampasi ya Dodoma 2013/2014 Bw. Remidius Emmanuel (kulia) akimpongeza  Bi. May  Issa kwa kufanya vizuri katika  masomo yake  kwa kipindi chote cha masomo yake.



No comments: