Wednesday, December 10, 2014

VETA WATAKIWA KUSIKILIZA MAONI YA WADAU WAO ILI KUJUA MAHITAJI YAO SANJARI NA KUBADILISHA MITAALA YA ELIMU

Na Woinde Shizza, Arusha 
 Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo hivyo ili kuendana na soko la ajira lililopo hivi sasa. 
 Hayo yanesemwa leo jijini hapa na Waziri  wa Kazi na Ajira  Mhe Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana 
 Mhe Kabaka aliwataka vijana kutumia fursa za kujiunga na Veta ili waweze kujiariri badala ya kufanya biashara za kuuza vitu mikononi bali watumie taaluma walizozipata kuzalisha vitu vyenye ubora. Alisema vijana wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi la vijana likiwa bado mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni vyema sasa vijana hao wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mbinu za kutengeneza vitu sambamba na kupata masoko ya uhakika.
Alisema ni vyema sasa Vyuo vya Veta vikaweka mkazo katika sekta ya madini na gesi ili waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu hiyo ambayo itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi wananchi. 
"Mahitaji ya vijana ni mengi katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kia sekta inamtegemea mtu fulani hivyo ni vyema Veta mkasikiliza mahitaji ya wadau sambamba na kutafuta mbinu za kufundisha zaidi ili kuendana na mahitaji ya soko na nyinyi vijana tokeni barabarani mkajiunge na vyuo vya ufundi ili kuweza kuuza biashara zenu kwa ubora badala ya kukimbilia kuuza barabarani ". Alisema Mhe Kabaka
Naye Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kongamano hilo hufanyika kila mwaka na kushirikisha wadau katika sekta mbalimbali ili kujadili masuala mbalimbali na mahitaji ya wadau hao katika sekta ya ajira sambamba na kuboresha mitaala itakayokwenda na wakati na kuwezesha vijana wanaopitia Veta kuwa bora zaidi kipindi cha kumaliza chuo na kupata ajira. 
Alisema pia Veta inakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha kwenye ujenzi wa vyuo vipya kwenye Wilaya mpya ambazo ni Katavi, Geita, Njombe na Simiu lakini pia kuonaongezeko kubwa la vijana na watu mbalimbali ambao wanajiunga na vyuo hivyo nchini kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali yanayowawezesha kupata ajira. 
 Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro alisisitiza kuwa Veta inatambua na kuthamini maeneo mbalimbali yanayohitaji soko la ajira ndio maana vijana wanaopata ujuzi kupitia veta wanafanya kazi kwa makini na kujipatia vipato zaidi. 
 Aliongeza kuwa hivi sasa Veta inashirikiana na tasisi na mashirika mbalimbali hususan ya sekta ya madini na gesi na kutoa mafunzo kwaajili ya kuwasaidia vijana kukabiliana na soko la ajira .


WAZIRI wa Kazi na Ajira Mhe.  Gaudensia Kabaka  wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao



Waziri wa ajira na kazi  Mhe. Gaudensia Kabaka akiwa katika picha ya pamoja wadau waliouthuria katika  konga mano hilo

Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa BG Tanzania Ms Kate Sullam anaemfatia ni Mr Jean Van Wetter ni mkurugenzi wa VSO Tanzania
Picha ya pamoja ya washiriki wa kongamono hilo wakiwa pamoja na Waziri wa ajira na kazi nje ya ukumbi wa hotel ya Naura Springs iliopo ndani ya jiji la Arusha
 Waziri  kabaka  wa kwanza kulia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi (hayupo pichani)  kuhusiana na
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)

 WAZIRI wa Kazi na Ajira  Mhe Gaudensia Kabaka  wakati alipokuwa akizindua kongamano
Baadhi ya waandishi  wakiendelea kufatilia kwa makini kongamano hilo
 Washiriki wakifuatilia

Kutoka  kulia ni mwenyekiti wa bodi ya veta Profesa Idrissa Mshoro wa pili kulia ni  Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi wakiwa wanamsikiliza waziri 

washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini


 Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi akiwa anaongea katika kongamano hilo
wadau kutoka sekta ya gesi na petrol wakiwa wanafatilia
Mada ikiwasilishwa

Wadau wakifuatilia mada 
waandishi  wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuoji mwenyekiti wa bodi

No comments: