Waziri
wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa
akifungua mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto za
utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote-EFA
uliofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu mwaka 2000
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuelekea kutimiza malengo ya Mpango
huo ikiwa ni utashi wa kisiasa na kuwajibika vikisaidiwa na kujitolea
kwa wadau wa sekta ya elimu pamoja na washirika wa maendeleo.(Picha na
Zainul Mzige wa MOblog).
Tanzania
imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini
mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa
wote (EFA).Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa
wadau wote wa elimu , Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini
Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa amesema Tanzania Bara na Visiwani
imeweza kukaribia kufikia malengo ya mpango huo ikiwa ni pamoja na suala
la wastani wa waalimu kwa wanafunzi.
Amesema
kwamba kwa shule za msingi Tanzania Bara imefikia wastani wa wanafunzi
47 kwa mwalimu mmoja wakati Visiwani Zanzibar ni wastani wa mwalimu
mmoja kwa wanafunzi 27. Mafanikio mengine yaliyopatikana chini ya mpango
huo ni kuboresha wastani wa wanafunzi kwa darasa, ambapo kwa Tanzania
Bara wastani umetoka kuwa wanafunzi 92 kwa darasa na sasa ni wanafunzi
65 huku Zanzibar wastani ukiwa ni wanafunzi 62 kwa darasa.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza wakati wa
mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto
zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu
kwa Wote –EFA ulioshirikisha wadau wote wa sekta ya elimu uliofanyika
jijini Dar Es Salaam. Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuiandaa
Tanzania kuweza kushiriki kikamilifu katika mashauriano ya kiserikali
baina nchi mbalimbali na kuhakikisha wadau wakuu wa elimu kitaifa
wanapata taarifa juu ya mapendekezo ya agenda zitakazoanza mwaka 2015.
Awali
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amesema
ikumbukwe kwamba malengo nane (8) ya EFA yanachangia kufanikisha Malengo
Makuu ya Maendeleo ya Millennia (MGDs) yaliyopitishwa mwaka 2000 kati
ya nchi 189 na Taasisi za Mendeleo zinazoongoza Duniani.
Bi.
Rodrigues amefafanua kuwa tunapoelekea mwaka 2015, Tanzania Bara na
Visiwani zimeonyesha juhudi katika kupunguza tofauti kubwa zilizokuwepo
kielimu ikiwa ni pamoja na kukabilia na changamoto zilizojitokeza na
kuweza kuweka sera, mipango na utawala bora katia Nyanja za fedha ,
wadau, usimamizi na uwajibikaji.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wadau wa elimu kutoka bara na visiwani
wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa mkutano wa kimataifa wa
kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza
malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA.
Katika
mkutano huo imeelezwa kwa sasa hakuna tatizo la uwiano wa wanafunzi wa
kike na wa kiume kwa kuwa jinsia zote zipo darasani katika uwiano
unaoridhisha unaokaribia wastani wa 50/50, lakini pia kigezo kingine ni
uwiano wa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari ambapo bado
kumeonyesha kuwa na mapungufu hivyo kazi ya ziada inahitajika.
Mkutano
huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na nia ya kutoa fursa kwa
nchi wahusika kujitathimini zimefikia wapi katika utekelezaji wa malengo
waliyojiweke ya Mpango wa Elimu kwa Wote-EFA kwa kipindi cha mwaka
2000 hadi 2015 na kujiwekea mikakati mipya.
Kamishna
wa Elimu kutoka Wizarani, Prof. Eustella Bhalalusesa (wa pili kushoto)
akitoa maoni juu changamoto zinazolikabili taifa katika kuleta uwiano
kwenye ya sekta elimu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akishea uzoefu wake katika
utekelezaji wa malengo ya EFA baina ya Tanzania na nchi zingine za
Afrika.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Maalim
Abdallah M. Abdallah (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mkutano huo. Kushoto
ni Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt.
Shukuru Kawambwa.
Waziri
wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania, Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa
akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira
Rodrigues baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Mkurugenzi
wa ofisi ya elimu kutoka Shirika la USAID, Bw. David Bruns (kushoto)
akibadilishana mawazo na Waziri Kawambwa (katikati) na Bi. Zulmira
Rodrigues.
Afisa
Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko akiteta jambo na
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta.
Waziri
wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru
Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana
na nafasi ya Tanzania ilipofikia tangu 2000-2015 katika utelekezaji wa
malengo ya EFA.
Afisa
mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akizungumza
na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa mkutano huo baina ya UNESCO na
Wizara katika kutathmini utelekezaji wa malengo ya EFA katika kipindi
cha miaka 15 na kutoa nafasi ya kujipanga kwa awamu nyingine itakayoanza
2015-2030.
No comments:
Post a Comment