Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Songambele (kulia), akionesha katiba ya chama hicho wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kupata viongozi wapya na mambo mengine. Kushoto ni Katibu wa TAPSEA, Festo Melkiory.
Makamu Mwenyekiti wa TAPSEA, Janejelly James (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Songambele (katikati) akiwa na viongozi wenzake, Kutoka kulia ni Mjumbe wa chama hicho, Godfrey Ngoloka, Makamu Mwenyekiti, Janejelly James, Katibu wa TAPSEA, Festo Melkiory na Marcelina Mshumbusi (Mjumbe).
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
UONGOZI mpya wa Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA), umejipanga kutatua kero na matatizo mbalimbali yanayo wakumba makatibu mahsusi nchini.
Akizungumza Dar es Salaam wakati akitambulisha uongozi wa awamu ya pili wa chama hicho ambao ulichaguliwa Julai mwaka huu, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Zuhura Songambele alisema uongozi huo mpya pia umejipanga kuhakikisha utekelezwaji wa sera ya ajira, fedha na utawala unafanyiwa kazi.
Alisema katika juhudi za kutatua kero hizo pia watahakikisha wanatokomeza unyanyasaji wa jinsia mbao umekuwa kero kwa makatibu mahususi wakiwa sehemu zao za kazi.
Songambele alitaja majina ya uongozi huo ni Zuhura Songambele, ambaye ni mwenyekiti, Makamu mwenyekiti Janejelly James, Katibu Festo Elikiory, Naibu katibu Rose Mwalimu.
Alitaja majina mengine ambayo ni ya wajumbe Monica Bayuni, Marcelina Mashumbusi, Catherine Mshatta, Atupakisye Mapuli, Vicky Eben, Godfrey Ngoloka, Fatma Kahungenge, Beatrice Mwasumbwi na Rose Kasiga.
Aliwataka makatibu mahsusi kujiunga na chama hicho ilikuweza kuwasilisha malalamiko yao na kuwa na sauti moja katika jamii na kuweza kuchukua hatua mbalimbali zitakazo wasaidia.
Alisema kuna zaidi ya makatibu 4000 nchini hivyo aliwataka waajiri kuwashawishi makatibu hao kujiunga na chama hicho ili kufanikisha mambo mbalimbali ya makatibu mahsusi.
No comments:
Post a Comment