Friday, December 26, 2014

PAMOJA NA MVUA KUBWA, TAMASHA LA KRISMAS LAACHA HISTORIA MJINI IRINGA

1Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akimtunza Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini DRC Congo wakati akiima kwenye tamasha la Krismasi lililofamyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wakiwemo Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Bony Mwaiteje, Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo, Solomon Mukubwa, Edson Mwasabwite Joshua Mlelwa, Ambwene Mwasongwe, Tumaini Njole, Emmanuel Mgogo na wengine wengi, hata hivyo mvua kubwa iliyonyesha mkoani Iringa imewafanya mashabiki wengi kutojitokeza katika tamasha hilo, Kundi zima la wanamuziki hao limekonga nyoyo za mashabiki mjini Iringa na linatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Songea mkoani Ruvuma ambapo tamasha kama hilo litafanyika Desemba 29 kwenye uwanja wa majimaji.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA) 2Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akicheza wakati mwimbaji Faraja Ntaboba akiimba kushoto ni mwimbaji Upendo Kilahiro akishiriki kucheza. 4Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba mbele ya mashabiki wake katika tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. 5Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba mbele ya mashabiki wake katika tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. 6
.17
Upendo Nkone kulia na Tumaini Njole wakicheza jukwaani.
19
Mwimbaji Bony Mwaitege akifanya vitu vyake jukwaani

No comments: