Monday, December 8, 2014

MAULID YA KUMPONGEZA BI. ZAHRA MUHIDIN MICHUZI YAFANA SANA

Ankal akimpongeza Binti yake Zahra wakati wa hafla ya Maulid ya Kumpongeza baada ya kulamba Nondozz yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii imefanyika jana Nyumbani kwa Kaka wa Ankal,Tabata Kimanga jijini Dar es salaam.

 Baba Mkubwa wa Zahra,Ismail Michuzi akiongoza dua ya kuwakumbuka ndugu waliotangulia mbele ya haki kabla ya shereha ya Maulid ya kumpongeza Binti Zahra alielamba Nondozz yake ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma,hivi karibuni.Kulia ni Ankal.
 Zahra akijumuika na Mashangazi zake katika Maulid hiyo

 Vijana wa Madrasa wakitoa burudani kwa Qaswida mwanana kabisa.
 Ankal akisikiliza Jambo kutoka kwa Kaka yake,Macheka.
 Dufu zikipigwa.
 Ankal akiwatunza vijana wa Madrasa.
 Vijana wa Madrasa wakiimba Qaswida kwa ustadi mkubwa.
 Zahra na Mama zake wadogo.
 Msimamo wa Qiyam.
 Shangwe zatawala.
 Binti wa Ankal,Zahra Muhidin Michuzi akiwa kaketi kwenye kiti chake tayari kwa kupongeza kwa kulamba Nondozz yake hiyo.
 Ankal na Dada yake,Bi. Ndonya

 Zahra katika picha ya pamoja na shangazi zake,Mama Zenna na Mama Fatma.







 Michuzi Famili
 Zahra na Marafiki zake.

 Ankal akiwa na Wanae,Ramadhan (pili kushoto),Zahra (kulia),Karim (kushoto) na Sellah (alie na Ankal) wakati wa hafla ya kumpoza Zahra alielamba Nondozz yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii ilifanyika Tabata kwa Kaka wa Ankal ambaye ni Baba Mkubwa wa kina Zahra.
Zahra akiwa na Wadogo zake Kulwa na Dotto ambao ni watoto wa Kaka Mkubwa wa Ankal.

8 comments:

Anonymous said...

Mabrooq kwa binti Michuzi. Anko umefanan sana na Zahra.

Anonymous said...

HONGERA SAANA DAZAHRA NONDOZ NI UFUNGUO WA MAISHA YENYE NEEMA
NAKUTAKIA KILA LA KHERI
Anko Mikidadi
DENMARK

Anonymous said...

Hongera sana Zahra kwa kula nondozz na Ankal kwa kumuwezesha binti.

Prof Julius and Mrs Alu Nyang'oro

Unknown said...

Hongera sana Zahra!
Sensei Romi.

Anonymous said...

What a nice family!

Anonymous said...

congrat bi zahra kwa kuhitimu masomo yako Mungu akuongoze ktk kila ujambo ufanyalo

Salum A. Nyamwese said...

Maashallah, Hongera Bi Zahra. Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi katika kuitumikia jamii yako kwa Elimu uliyoipata. Kumbuka hiyo ni Dhamana Familia inakutegemea, Taifa linakutegemea na Dunia kwa ujumla wake inategemea kuletewa mabadiliko na wewe. Hongera sana.

Say
Salum Nyamwese
FUN OF MICHUZI BLOG.

Fadhiri Atick said...

Mmemeremeta sana,hongera dada Zahra