Saturday, December 6, 2014

MASHINDANO YA WAZI YA UBINGWA WA TAIFA YANAVYO ENDELEA KATIKA UWANJA WA NDANI WA TAIFA

Bondia Abuu Said wa JKT akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Adolf Emanuel wa Kigoma wakati wa mashindano ya wazi ya Taifa ya masumbwi yanayoendelea katika Uwanja wa ndani wa Taifa.  Said alishinda mpambano huo na kuingia fainali 
Uringo mpya wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT waliopewa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel hivi karibuni wakiufanyia majaribio ya kuuchezeshea ngumi kabla ya makabidhiano rasmi na kampuni hiyo
Baadhi ya viongozi wa mchezo wa ngumi nichini wakifuraia jambo wakati wa mashindano ya taifa ya ngumi yanayo endelea katika uwanja wa ndano wa taifa kutoka kushoto ni Meja Rodgers Daudi  ambae pia ni refarii na jaji wa mchezo wa masumbwi Mjumbe wa maendeleo ya wanawake  BFT Aisha Voniatis  na Katibu mkuu wa chama hicho Makore Mashaga 


VIONGOZI WAKIFUATILIA   MCHEZO WA MASUMBWI UNAVYO ENDELEA
Mabondia Bosco Bakari wa JKT  kushoto akioneshana umwamba kutupiana makonde na Athanas Emmanuel wa Kigoma wakati wa mashindano ya wazi ya taifa yanayoenderea katika uwanja wa ndani wa taifa 
Wadau wa mchezo wa masumbwi nchini wakipiga picha mbele ya uringo mpya wa BFT kutoka kushoto ni Mjumbe wa maendeleo ya wanawake  BFT Aisha Voniatis. Rais wa TPBO Ustaadh na mdau mkubwa wa mchezo wa masumbwi nchini SUPER DIEGO wa Mapambano
Mabondia Babu Luda wa Morogoro  kushoto na Victor Njaiti wa JKT wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya wazi ya ubingwa wa taifa yanayo enderea uwanja wa ndani wa Taifa. Njaiti alishinda mpambano huo na kuingia fainali 
Bondia Fred Julius wa Kigoma  kushoto akitupiana makonde  na  Robert Kyaruzi wa Bukoba wakati wa mashindano ya Taifa ya mchezo wa masumbwi nchini yanayo enderea katika uwanja wa ndani wa Taifa Kyaruzi alishinda kwa KO ya raundi ya pili 
Mabondia Babu Luda wa Morogoro  kushoto na Victor Njaiti wa JKT wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya wazi ya ubingwa wa taifa yanayo enderea uwanja wa ndani wa taifa Njaiti alishinda mpambano huo na kuingia fainali. 

No comments: