Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akimkabidhi, Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa (kulia), bati na rangi zenye thamani ya sh.milioni 3.5 zilizotolewa na mfuko huo jana, kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara. Anayeshuhudia makabidhiano hayo katikati ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha wakati akikabidhi msaada huo. Kulia ni Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.
Hapa ni kubadilishana mawazo baada ya makabidhiano hayo.
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Jengo la maabara la shule hiyo lililokamilika ujenzi wake.
Jengo la maabara ambalo ujenzi wake unaendelea.
Baadhi ya majengo ya shule hiyo yanvyoonekana.
Jengo la utawala la shule hiyo.
Dotto Mwaibale
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umeunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.milioni 3.5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mlandizi wilayani humo jana, Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo, Isaya Mwakifulefule alisema mfuko huo umejiwekea utaratibu wa kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika shughuli za maendeleo ya kijamii.
"Mfuko wetu kila kanda nchini wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na katika hilo mnaweza kuwa mashuhuda kwani siku za hivi karibuni mmeweza kuona tulivyotoa msaada kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (albino)" alisema Mwakifulefule.
Alisema ujenzi maabara katika shule hapa nchini ni muhimu sana katika wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia ambapo wanahitaji wanayansi wengi kwa utaalamu wa aina mbalimbali hasa katika masuala ya utafiti.
Alitaja vifaa vilivyotolewa na mfuko huo kuwa ni mabati na rangi kwa ajili ya kukamilishia ujenzi wa maabara hizo na alitoa mwito kwa wadau wa maendeleo na mifuko mingine kujitokeza kusaidia eneo hilo kwani kuna mahitaji makubwa ya maabara nchini.
Akipokea msaada huo kwa niana ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa wilaya hiyo, Doris Semkiwa alisema msaada huo utapunguza changamoto ya ujenzi wa maabara kwenye shule hiyo.
Alisema ujenzi wa maabara katika wilaya hiyo umekamilika kwa asilimia 67 na kuwa ujenzi huo unaendelea kwa kasi ambapo wanatarajia kukamilisha kazi hiyo mapema iwezekanavyo.
Alisema kwa wilaya nzima yenye shule za sekondari 8 mahitaji ni kuwa na maabara 24 na tayari wamejenga 14 na kuwa fedha zinazotumika kwa ujenzi huo zinatoka katika mapato ya ndani ya Halmshauri, wadau mbalimbali na nguvu za wananchi.
Aliongeza kuwa ujenzi huo utagharimu zaidi ya sh, milioni 400 na kuwa changamoto kubwa ni mapato ya ndani kuwa kiduchu na kuwa kama wangekuwa na fedha za kutosha wangeweza kumaliza kwa wakati ujenzi huo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha aliwashuku LAPF kwa msaada huo pamoja na Halmsahauri kwa fedha za luzuku inazozitoa kila mwezi kusaidia mambo mbalimbali katika shule hiyo na zingine sanjari na ujenzi wa maabara hizo.
"Naishukuru Halmshauri kwa fedha hizo ambazo imekuwa ikitupa kila mwezi kusaidia katika maeneo mbalimbali" alisema Masha.
No comments:
Post a Comment