Afisa
Habari wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mkoani Kilimanjaro
(KWIECO), Veronica Ollomi akifafanua jambo katika Warsha ya siku mbili
kwa waandishi wa Habari wa mkoa wa Kilimanjaro, kilichofanyika
juzi mjini Moshi, kwa lengo la kuwapa mafunzo juu ya Haki za Binadamu
na Sheria zake.
Washiriki wa Warsha ya Haki za Binadamu, waandishi wa
Habari mkoani Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini wakati wa
uwasilishaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo, yakiwemo swala la
Wosia, Sheria ya Ardhi kwa Lengo la kuwawezesha kupata uelewa wa
sheria hizo katika utendaji wao wa kazi.
Mtangazaji wa Redio Moshi FM, Neema Mkotya akiweka
sawa mitambo kabla ya kuwasilisha Mada.
Mtaalamu wa maswala ya Haki za Binadamu kutoka
KWIECO, Elizabeth Mushi akifafanua jambo kwa washiriki wa Warsha
hiyo.
Waandishi wa Habari, Heckton Chuwa (Bussiness times),
Nakajumo James (Habari Leo) na Happiness Tesha (Raia Tanzania)
wakifuatilia mafunzo.
Sehemu
ya Washiriki wa Warsha ya Haki za Binadamu, Waandishi wa Habari wa
mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia uwasilishaji wa Mada katika Warsha
hiyo.
Mwezeshaji Elizabeth Mushi akiendelea na Uwasilishaji wa
Mada mbalimbali katika Warsha hiyo
Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Johnson Jabir,
akiwasilisha kazi iliyofanywa na kundi lake kwa niaba ya
wenzake.
Na
Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii Kanda ya Kaskazini
No comments:
Post a Comment