Walemavu wakiwa katika maandamano yao leo
Askari wa usalama barabara Iringa aliyefahamika kwa jina la Sarehe
Mollel akiongoza maandamano ya watu wenye ulemavu leo wakati wa
maadhimisho ya siku ya walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika
viwanja vya kichangani mjini Iringa na kuhudhuriwa na waziri wa nchi
ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi kwa
niaba ya waziri mkuu Mizengo Pinda
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Bw
Wiliam Lukuvi akimkabidhi cheti cha ushiriki Tumain Mdegella kwa niaba
ya ofisi za Neema Crafti mjini Iringa wakati wa kilele cha
maadhimisho ya siku ya walemavu duniani iliyofanyika kitaifa mjini
Iringa
Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI
imeziagiza mamlaka za usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA )
nchini kuanza mchakato wa kukaa na wamiliki wa vyombo hivyo ili
kuanza uangizaji wa vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi ambayo ni
rafiki na walemavu nchini huku ikipiga marufuku majengo ya serikali
kujengwa bila kuwepo kwa mchoro unaoonyesha mazingira yanayozingatia
makundi yote ya jamii likiwemo la walemavu wa viungo .
Agizo
hilo limetolewa na waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa maadhimisho
ya siku ya walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika
viwanja vya kichangani mkoani Iringa jana.
Akiwahutubia
walemavu hao na wananchi waliofika katika viwanja hivyo waziri
mkuu ,aliyewakilishwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na
uratibu wa bunge) ,Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa jimbo la Isimani
mkoani Iringa alisema kuwa kimekuwepo kilio cha muda mwingi kutoka
kwa walemavu juu ya kusaulika katika ujenzi wa majengo mbali mbali
ambayo yamekuwa yakijengwa bila kuzingatia kundi la watu wenye
ulemavu jambo ambalo ni sawa na kuwabagua watu hao.
Hivyo
alisema katika kuona kilio hicho cha walemavu kinafanyiwa kazi
kuanzia sasa majengo yote ya serikali zikiwemo shule na taasisi
nyingine kabla ya kuanza ujenzi wake lazima wasimamizi wa ujenzi
huo kujiridhisha kwa mchoro ambao utaonyesha mazingira
yatakayomuwezesha mlemavu kutumia jingo hilo bila usumbufu tofauti
na ilivyo sasa ambapo idadi kubwa ya majengo mazingira yake si
lafiki kwa walemavu.
"
Ni siku nyingi watu wenye ulemavu wamekuwa wakilalamika juu ya
mazingira yasiyo rafiki katika majengo mbali mbali .....sasa leo
naomba kuagiza kuwa michoro yote inayochorwa katika majengo ya huduma
za kijamii ni marufuku kupitishwa ama wasimamizi wa ujenzi
husika kuruhusu ujenzi iwapo mchoro hauonyeshi kama utayajali
makundi yote wakiwemo walemavu.....wasimamizi wote msikubali
kusimamia wala kutangaza tenda ya ujenzi kama ramani yake si
rafiki kwa walemavu.....lakini pia hata kwenye mabasi hivi
unamtegemea mtu mwenye ulemavu wa miguu ataingia vipi na baiskeli yake
katika gari iwapo hakuna mazingira yanayomwezesha kuingia ....hivi
sasa teknlojia imezidi kukua na baadhi ya nchi wameanza muda mrefu
kuwajali walemavu kwa kuwa na mabasi ambayo mlemavu anaingia na
baiskeli yake na kushuka nayo bila usumbufu ni vema hata Sumatra
kuangalia uwezekano wa kuwajali walemavu hao . pia ni vizuri hata
nyumba za ibada nazo ningeshauri baba askofu kuangalia kuweka
mazingira " alisema Lukuvi.
Kuhusu
ombi la walemavu hao hasa wale wasio sikia kuomba serikali kuwa
na wakalimani katika kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na vituo
vingine vya luninga ili kuwawezesha walemavu hao nao kuweza
kufuatilia hotuba ya Rais mwisho wa mwezi na mambo mengine badala ya
kutengwa ,alisema kuwa suala hilo ni wajibu wa serikali kuwajali
watu wake hivyo tayari imeuagiza uongozi wa TBC na mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA) kulitafutia ufumbuzi suala hilo la
mkalimani hasa katika TBC .
Katika
hatua nyingine Lukuvi aliwataka walemavu hao ili ombi lao la
kutazamwa katika nafasi za uongozi liweze kuzingatiwa ni vema wao
wenyewe kujitokeza kwa wingi kuipigia kura katiba iliyopendekezwa
pindi itakapokuja kwa wananchi kwa madai kuwa katika katiba hiyo
imezingatia mambo mengi ya kijamii likiwemo la kuwajali watu wenye
ulemavu kwa kuwatengea nafasi nyingi zaidi na iwapo katiba hiyo
itapitishwa kazi ya msuguano wa rushwa unaweza kuhamia kwa walemavu
kwa kila mmoja kutaka kupewa nafasi.
"
Hadi hivi sasa ni chama cha mapinduzi (CCM) pekee ambacho kina
wabunge wa viti maalum wa kuteuliwa kutoka kundi la walemavu huku
vyama vingine vyote havijawakumbuka kabisa watu wenye ulemavu
ukiacha mbunge wa jimbo la Lindi mjini pekee ambae hakupendelewa
katika ubunge wake bali alishindwa kihalali kwa kuchaguliwa na
wananchi wake..nafikiri tushirikiane kuhakikisha katiba hii
iliyopendekezwa inapita ili tuungane pamoja katika kujenga nchi
yetu "
Katika
salam za walemavu waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dkt Seil S.
Rashid zilizotolewa kwa niaba yake na mwenyekiti wa baraza la
watu wenye ulemavu nchini na Dunford Makala alisema
kuwa wizara inaendelea kuimarisha ushirikiano na vyama vya watu
wenye ulemavu na shirikiasho la vyama vya watu wenye ulemavu
Tanzania (SHIVYAWATA) katika kuhakikisha utekelezaji wa uwekaji wa
fursa na haki sawa kwa watu wenye ulemavu nchini .
Alisema
katika kuhakikisha ushirikiano unakuwepo wizara yake imezindua
baraza la ushauri la Taifa la watu wenye ulemavu toka mnamo 1
Novemba 2014 na katika hilo kamwe hawataacha kumpongeza Rais Dkt
Jakaya Kikwete kwa kumteua mwenyekiti wa baraza hilo.
Aidha
alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa nchi hii chini ya Rais Dkt
Kikwete imefanya mambo mengi zaidi ya kuwajali watu wenye
ulemavu katika Nyanja za kiuchumi ,kiutamaduni na kisiasa ambavyo
vyote hivyo kumwezesha mlemavu kujikwamua kimaisha.
Hata
hivyo alisema ushahidi wa yote hayo ni pamoja na kuridhia mikataba
ya kimataifa juu ya haki za watu wenye ulemavu , kutungwa kwa sharia
Na.9 ya mwaka 2010 ya watu wenye ulemavu na kanuni zake
,kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika tume ya mabadiliko ya
katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na kuteuliwa kwa
wajumbe 20 wenye ulemavu katika bunge maalumu la mabadiliko ya katiba
la mwaka 2014.
Awali
walemavu hao katika risala yao iliyosomwa na makamu mwenyekiti wa
SHIVYAWATA Amina Mollel pamoja na kuishukuru serikali kwa jinsi
kwa kuendelea kuwa karibu zaidi na watu wenye ulemavu kwa kushiriki
shughuli mbali mbali za walemavu ,bado waliweza kuishukuru serikali
kwa kuandaa sera ya maendeleo ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004,
kutambuliwa kwa watu wenye ulemavu katika MKUKUTA,kuwezesha kuongezeka
kwa idadi ya watu wenye ulemavu wanaopata elimu kuanzia shule za
msingi hadi elimu ya juu na mambo mengine mengi ambayo wao kama
walemavu wamekuwa wakiona serikali yao ipo pamoja nao.
Sanjari
na mema hayo bado waliiomba serikali kuzingatia kuwapatia walemavu
mambo muhimu katika maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuwa na
vyombo vya usafiri rafiki kama magari moshi.vyombo vya usafiri majini
,angani ,miundo mbinu katika majengo na viwanja vya ndege ambavyo
vitamwezesha mlemavu pia kuwa huru.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa maadhimisho hayo
yaliyofanyika chini ya kauli mbiu isemayo " Maendeleo endelevu
;Ahadi ya Teknolojia huku mkoa wa Iringa ukiendelea kuwa bega
kwa bega na walemavu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi karibu na
vyama hivyo vya watu wenye ulemavu na kuwa mkoa huo kwa sasa
una jumla ya walemavu zaidi ya 179 ,000 na wote serikali
imeendelea kuwalinda na kuwa nao pamoja.
|
No comments:
Post a Comment