Wachezaji
wa timu ya Chuo cha Sayansi za Jamii, wakijifua kwa mazoezi kabla ya
mchezo wao dhidi ya timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia katika
fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni
255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam
juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo,
uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosaa taa.
Wachezaji wa timu za Chuo cha Sayansi za Jamii (jezi nyeusi) na Chuo
cha Uhandisi na Teknolojia, wakigombea mpira wakati wa mchezo wa fainali
ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255,
yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi.
Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika
kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram
Mapunda akikagua wachezaji wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, kabla ya
kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia
huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu
jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika
mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufuatia giza kuingia na uwanja
kukosa taa.Kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
Kaimu
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda
akikagua wachezaji wa Chuo cha Sayansi za Jamii, kabla ya kuanza kwa
mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya
Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo,
uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa.
====== ====== ========
Fainali
ya Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) yanayojulikana kama Airtel UNI255 yaliyoshirikisha
wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo chuoni hapo yamemalizika
siku ya jumamosi ya tarehe 13/12/2014 Katika Fainali iliyovikutanisha
vyuo vya Sayansi ya Jamii(College of Social Science)na Chuo cha Uhandisi
na Teknolojia (College of Engineering and Technology) ambapo hadi
dakika tisini(90) zinamalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam(UDSM) zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Timu
ya kitivo cha CoET iliyokua na upinzani mkali kwa jumla ndiyo iliyokuwa
ya kwanza kupata bao dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza mfungaji akiwa
ni Justin Rupia kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa CoSS
Chawaka Francis na kumfanya mwamuzi wa mpambano huo Wema Ngota pamoja na
wasaidizi wake Benjamini Mbughi, Hellen Mduma, Iddi Mfaume, Ramadhan
Pondamali,Jackison Msilombo, Ally Sarehe na Faraji Gaibu,walioichezesha
michezo hiyo tangu tarehe 8 mwezi huu kuwa katika hali tete kutokana na
shangwe, nderemo na vifijo kutoka kwa Mashabiki wa CoET kucharuka uwanja
mzima.
Kipindi
cha Pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo CoSS iliwatoa Emmanuel
George na Morrison Ng’owo na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji Rashidi
Hussen na Ramadhan Hussen dakika ya 67 na 75 huku wenzao wa kitivo cha
CoET aliingia mchezajji Tibe Mario kuchukua nafasi ya mchezaji George
Michael katika dakika ya 62 mabadiliko yaliyowanufaisha zaidi CoSS
waliposawazisha bao dakika za Majeruhi baada ya kutokea piga nikupige na
hivyo kuleta mtafaruku kutokana na Muda(Kiza) kuingia ambapo timu hizo
zilishindwa kupigiana Penalti ili kupata mshindi wa kwanza na mshindi wa
pili.
Katika
michezo ya awali timu hizo za College of Social Science waliokuwa kundi
B lililokuwa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama
Mabibo Hostel ilifanikiwa kuongoza vizuri ambapo ilicheza mechi 3
ikashinda moja na kutoa sare ya bila kufungana mechi 2. matokeo
yalioyowapa pointi 5 na goli 2 na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali.
Katika
michezo ya awali timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia-College of
Engineering and Technology(CoET) iliyokuwa kundi A lililokuwa katika
viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) ilifanikiwa kuongoza pia
vizuri na kupata pointi zilizoiweka kwenye nafasi ya kucheza Fainali
baada ya kushinda hatua ya nusu fainali dhi ya timu ya UDBS.
Timu
iliyochukua nafasi ya tatu ni kitivo cha UDBS waliofanikiwa kuwafunga
Kitivo cha SoED kwa njia ya penalty baada ya kumaliza dakika 90 kwa
kufungana 2-2 katika mchezo uliokuwa wa upinzani mkubwa kutokana na timu
ya SoED kuwa na wachezaji wengi wakongwe waliokaa muda mrefu hapo
chuoni na wameshiriki michuano mingi na wamefanya vizuri na ndiyo timu
pekee iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kunyakua Uchampioni huo wa Chuo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti timu Capateni wa Timu zilizoshiriki hatua ya nusu
fainali, Bodoo Oduon wa Timu ya CoET, Michezo hiyo imeleta changamoto
kubwa kwa wanafunzi na kuwataka wadhamini kujitokeza kudhamini michezo
ya vyuo vya mkoa wa Dar es Salaam.
“Tumefurahi
pamoja, tumecheza na kuruka ruka hii ni shangwe, tena mimi nasema hawa
Airtel hakika wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa, ni pesa ngapi wamewekeza
hapa, na hii ni kwa Chuo Kimoja tu ch UDSM na bado kuna hiyo michuano ya
vyuo vya Dar es Salaam, ni muunganiko mzuri unaoletwa na hawa Airtel
kwa kutuunganisha kati ya vyuo na vyuo”alisema Bodoo Oduon.
Kuhusu
kutopata matokeo ya Mshindi wa kwanza timu kampteni wa CoSS Elias
Mshomba alisema kuwa ni kawaida kutokea jambo hilo, maana Fainali
ilihusisha watoto wa baba mmoja, kwamba jambo kubwa ni juu ya hizo
College zilizoingia fainali kuwa wawakilishi wa College Championship Dar
es Salaam inayotazamiwa kuunguruma mapema kuanzia mwezi wa tatu
mwakani.
“Wewe
unadhani kuna jambo limeharibika hapa kwa kutopata mshindi wa kwanza
ama wa pili, sisi tulikuwa katika mchujo wa kupata wawakilishi wa chuo,
kama ni zawadi zote ni za UDSM, hivyo nawaomba wachezaji wote
waliofanikiwa kuzifikisha timu zao hatua ya nusu fainali, kuendelea na
maandalizi makali ya kuhakikisha tunatwaa hizo zawadi zinazokuja za
ushindani wa vyuo vya Dar es Salaam, mwenyewe umeona kiza kimeingia
hivyo wachezaji wasingekuwa na uwezo wa kumaliza penalty tano kabla ya
usiku na hapa hakuna taa, tusubiri hiyo michuano ambayo sijui wadhamini
ni nani kama watakuwa ni Airtel basi itakuwa Raha sana maana
tumefurahishwa na Airtel” alisema Elias Mshomba.
Akiongea
kuhusiana na mwenendo wa mashindano hayo kwa Waziri wa michezo wa
jumuiya ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema
“Mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na
wadhamini wetu Airtel kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja
yameongeza hari sana kwa washiriki wote, na Pengine hii imekuwa ni
changamoto kwetu kutokana na Uwepo wa Michuano ya Wanavyuo, College
Championship Tanzania” alisema.
Na
kuongeza kuwa “sisi kama UDSM tumepewa heshima kubwa ya kutoa
wawakilishi wane watakaoungana na College zingine Kuunda jumla ya Timu
32 za College Kanda ya Mashariki,hivyo tumefaidika sana sisi kama chuo,
kwa kuwa jambo lingine tumeweza kufanya Selection (Usahili) wa kupata
timu ya chuo (UDSM ALLY STARS)ambayo inaweza kuwakilisha chuo kwenye
michezo ya EAST AFRICAN UNIVERSITIES COMPETITION, inayoshirikisha nchi
za Afrika mashariki kwa michezo ya Vyuo Vikuu,lakini pia nichukue Fulsa
hii kuwaomba tena Airtel, kupitia hii hii Airtel UNI255 kuweza kudhamini
hatua inayofuata ya Michezo ya Vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, NACTE
& Inter College Championship-Dar es Salaam,itakayoshirikisha jumla
ya vyuo 32, Kama ulivyoona mwenyewe jinsi ushindani ulivyomkubwa na hata
soka lenyewe lipo vyuoni,shamra shamra zote hizi hapa ni chuo kimoja je
itakapokuwa imekutanisha vyuo vingine kama vile
IFM,DIT,NIT,TRA,ISW,IAE, BANDARI COLLEGE,CBE, DACICO, HEDEN HILL,
NJUWENI, MUHIMBILI MEDICAL SCHOOLS, KIBAHA COTC na St. JOSEPH UNIVERSITY
ambazo tayari zimefuzu hatua ya Makundi yake ya Michuano ya Bonanza la
NACTE INTER COLLEGE DAR ES SALAAM BONANZA unadhani shamra shamra
zitakuwaje, na tunaomba hiyo Fainali ya College za Dar es Salaam
ifanyike Uwanja wa Taifa ili TFF na Makocha wa Timu ya Taifa waje
wachague wachezaji watakaoisaidia Tanzania katika michuano ya Taifa na
kimataifa”alisema STANLRY.
Timu
iliyoonyesha nidhamu na Ushindani mkubwa wa kuwania hizo nafasi wakati
wa mchujo huo wa College ya UDSM ili kuingia kwenye ushiriki wa
michuano ya Vyuo vya Dar es Salaam ni SJMC iliyokuwa kinara wa kundi A
katika viwanja vya ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaa ni (School of
Journalism and Mass Communication) ilicheza mechi mbili na kushinda zote
na kujitengenezea pointi 6 na huku akiongoza kwa kuwa na bao 5 za
kufunga.
Akizungumzia
michezo hiyo kwa upande wa College za UDSM mratibu wa College za chuo
hicho bwana. Albert Kimaro alisema kuwa “ Kundi B ambalo mechi zake
zilichezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo
Hostel, ndilo lililokuwa na timu zenye wachezaji wakongwe na liliongozwa
na COSS (College of Social Science) timu iliyokuwa na mashabiki wengi
na ambayo imeweza kucheza Fainali, lakini pia ndani ya UDSM zimeshiriki
College kama CONAS, ambayo pia ilikuwa na wachezaji wazuri, UDSL, COET,
COICT,ISK,na COHU” alisema Albert.
Mgeni
Rasmi katika Fainali hiyo Profesa Mapunda Mapunda baada ya ukaguzi wa
wachezaji aliwaasa kuwa na utulivu, Upendo, mshikamano, wakati wote wa
michezo na waepuke ugomvi wakati wote kwani michezo ujenga na kuimarisha
mahusiano mwao.
“kikubwa
hapa ni jinsi ya kujenga misingi imara ya michezo ndani ya vyuo vyetu,
sina maana katika chuo hiki pekee, bali vyuo vyetu vyote, lakini pia
niseme kwamba miaka ya nyumba hatukuwa na hamasa ya michezo vyuoni
kutokana na miundo mbinu, lakini wakati huu nadhani kwamba michezo ama
vipaji vipo vingi vyuoni, nimesikia kuna kampuni ya MIDETA entertainment
imeanza harakati za kuanzisha hii michezo ya vyuo vyote vya Dar es
Salaam na Tanzania kwa ujumla,inayojulikana kama College Championship
Dar es Salaam, ambapo kwa sasa kuna mtowano mwingine unaendelea wa vyuo
vingine kupitia mfumo uliowekwa wa Bonanza la Nacte inter College Dar Es
Salaam ili kupata timu zitakazoshiriki ligi hiyo itakayokuwa na timu
32, nina hakika kwamba michuano itakuwa mizuri na itapendwa sana na pia
itazalisha vijana wengi watakaokuwa wasomi kasha wawakilishi wetu
kimichezo” alisema Profesa Mapunda.
Naye
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackison Mbando alisema kuwa kuwa Mashindano
yalikuwa mazuri na timu na kwamba imewapa changamoto ya kuongeza
udhamini kwenye michezo ya vyuo, “ kama unavyoona mwenye jinsi Fainali
ilivyosheheni watu utadhani mechi yay a Mtani Jembe, upinzani ni mkubwa
sana na imeleta changamoto sana, lakini kubwa ni kuhakikisha kwamba
Airtel inawafikia Watu wote kwa namna ya pekee,
Tupo
katika harakati za kuboresha maisha ya wanavyuo kwani tunatambua kwamba
wanahitaji kusoma kwa kutumia Mitandao katika ulimwengu huu wa sasa
ambao Airtel kama unavyoona ni zaidi ya mitandao mingine, tunaanza sisi
kisha wanafuata wengine nah ii tumeanza kwa kuwa karibu na wanavyuo ili
tuwape nafuu katika usomaji na upataji wa mawasiliano, lakini si hivyo
tu kama unavyoona hapa leo mambo yamenoga katika kuwapa pia afya
wanafunzi wa vyuo kwani Michezo inaleta afya ndiyo maana tumeamua
kuingia sasa kusaidia na kudhamini hii michezo ya Vyuo, na sasa tumeanza
na College za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tunatarajia kufanya
mazungumzo na waandaaji wa Michezo ya vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam
(MIDETA entertainment) tupate mahitaji yao tuangalie, uwezekano upo wao
waje tuzungumze na ikibidi hata kupata timu bora ya College za
Tanzania,(College Championship Tanzania”alisema Jackison Mbando.
Aidha
katika kilele cha tamasha hilo Airtel ilizindua kwa wanafunzi wa chuo
kikuu huduma ya UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet
kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment