Monday, November 17, 2014

WAZIRI MEMBE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU SAYANSI YA JAMII

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba ya ufunguzi wa   Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii. Mkutano  huo ambao unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani  chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawashirikisha Wajumbe kutoka  Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, Nigeria na Canada. Katika hotuba yake Mhe. Membe alisisitiza umuhimu wa Wasomi na Wanazuoni kujikita katika Tafiti za Kisayansi ili kuja na majibu yatakayoisaidia nchi kuondokana na umaskini, utunzaji wa mazingira na masuala mengine ya manufaa kwa nchi.
Mhe. Membe akikaribishwa na Prof. Florence Luoga ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii  ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Mhe. Membe akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano huo
JUU NA CHINI: Ni sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mkutano huo kuhusu masuala ya Sayansi ya Jamii.
Mhe. Membe akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi huku wajumbe wakimsikiliza.
Sehemu ya wajumbe wakifurahia jambo wakati Mhe. Membe (hayupo pichani) akitoa hatuba ya ufunguzi.
Mhe. Membe akisindikizwa kwenda kupiga picha ya pamoja na Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwepo kwenye mkutano huo
Mhe. Membe (wa tatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano kuhusu masuala
Waziri Membe akifurahia jambo na mmoja wa Wajumbe wanaoshiriki mkutano huo.
Mhe. Membe akihojiwa na Wanahabari kuhusu mkutano huo. Picha na Reuben Mchome

No comments: