Wafanyakazi
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),leo Novemba 18,2014 walitembelea
Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,ambapo waliweza kutoa
msaada wa vitu mbali mbali kwa watoto waliolazwa Hospitalini hapo pamoja
na kukabidhi baadhi ya vifaa vya Usafi kwa Uongozi wa hospitali hiyo
Mbali na kukabidhi vifaa hivyo,pia walijumuika pamoja na kujitolea
kufanya usafi wa Mazingira ya Hospitali hiyo.
Mara
baada ya kukamilisha shughuli zote za hospitalini hapo,Wafanyakazi hao
walielekea moja kwa moja katika Shule ya Msingi Misitu,ilipo katika Kata
ya Kivule,Kitunda na kuweza kukabidhi msaada wa Madawati 100 ambayo
yatapunguza adha ya kukaa chini kwa asilimia 74 ya wanafunzi wote wa
shule hiyo ambao idadi yake imefikia 590.
Hapo awali wanafunzi hao wote walikuwa wakikaa chini na kuendelea na masomo yao.
TRA imefikia kufanya hivyo,ikiwa katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi chenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" ambayo kilele chake ni Novemba 21,2014 huku Mgeni Rasmi akitazamiwa kuwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakijadiliana
jambo wakati wakijiandaa kwenda kufanya usafi wa Mazingira wa Hospitali
ya Temeke,Jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2014.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiendelea kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo mbali mbali Hospitali ya Temeke,Jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2014.
Meneja wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Temeke,Victor Msuya (kulia)
akizungumza na mmoja wa wauguzi wa zamu katika Wadi ya Watoto ya Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Novemba 18,2014,wati Timu TRA ilipotembelea Wadi hiyo.
Baadhi ya Watoto waliolazwa kwenye Wadi hiyo.
Daktari
akichukua vipimo kwa mmoja wa watoto waliolazwa kwenye Wadi ya Watoto
ya Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam huku mzazi wake
akimuangalia.
Meneja wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Temeke,Victor Msuya (kulia)
akiwaongoza maafisa wengine wa TRA kutoa bidhaa mbali mbali walizokwenda
kuwagawia watoto wanaopatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Temeke,Jijini
Dar es Salaam leo Novemba 18,2014.
Sehemu
ya Maafisa wa TRA wakiwa nje ya jengo la Hospitali ya Temeka mara baada
ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira wa Hospitali hiyo.
Meneja
wa Wagonjwa waliolazwa wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke,Nuswe Ambokile
akizungumza na wanahabari wakati akitoa shukrani kwa Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa
kuweza kujitoa kwao kwenda Hospitalini hapo na kutoa msaada
waliofanikiwa kuutoa na kujitolea kwao kufanya usafi wa mazingira.
Picha ya pamoja.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Misitu,Ilipo katika kata ya
Kivule,Kitunda jijini Dar es Salaam wakiwa wameketi kwenye madawati
mapya yaliyokabidhiwa leo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Nyuma yao
ni Baadhi ya Maofisa wa TRA waliofika shuleni hapo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Misitu,Hyasinta Hugo akizungumza wakati
akiukaribisha Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Shuleni hapo.
Mkurugenzi
wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard
Kayombo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki kuzungumza na uongozi
wa Shule hiyo na kukabidhi madawati.
Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki
akizungumza na uongozi wa Shule hiyo pamoja na wanafunzi kabla ya
kukabidhi madawati,yaliyotolewa na TRA kwa shule hiyo.
Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki
akizungumza na wanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Misitu.
Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki
akipena mkoni na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misitu,Hyasinta Hugo
wakati akimkabidhi madawati 100 yaliyotolewa na TRA kwa shule hiyo.
Diwani
wa Kata ya Kivule,Mh. Nyasika Motewa akitoa shukrani zake za dhati kwa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mchango wao huo kwa Shule ya Msingi
Misitu iliopo kwenye Kata yake.
Sehemu
ya wanafunzi wa Shule hiyo ya Misitu wamkisikiliza kwa makini Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo akitoa Shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa hapo awali,kabla TRA hawajapeleka madawati shuleni hapo.
Wanafunzi wakiendelea na masomo.
No comments:
Post a Comment