Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa
wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini
linalotarajiwa kuanza Novemba 10 katika halmashauri 16. Wengine (walioketi) ni
Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya Wambura (wa pili kushoto), meneja
masijala ya walengwa Philipine Mmari (wa kwanza kushoto), Mtaalamu wa Mafunzo
Mercy Mandawa (wa pili kulia) na Meneja Rasilimali watu Tecla Makundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiri wa mafunzo kwa
wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini.
Afisa Ufuatiliaji na tathmini wa TASAF Bw. Paul Luchemba akitoa
mada juu ya malengo ya warsha ya mafunzo
kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini katika
ukumbi wa AMECEA Kurasini Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa
kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kupitia Mpango wa kunusuru kaya
maskini PSSN wakifuatilia mjadala baada
ya uwasilishaji wa madajuu ya mwongozo wa mpango katika ukumbi wa TEC-Kurasini
jijini DSM
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa
kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini
PSSN wakifuatilia maelekezo toka kwa wawezeshaji.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa
kaya maskini unaotekelezwa na TASAF wakisikiliza
mada zinazowasilishwa na wawezeshaji wa warsha hiyo kwenye ukumbi wa TEC jijini
DSM. .
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa
neno la ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa (hawapo
pichani) kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kuanza Novemba
10 katika halmashauri 16 nchini . Aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya
Wambura.
TASAF YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI NGAZI YA TAIFA KUHUSU
TUKIO LA UTAMBUZI WA KAYA MASKINI UKUMBI WA TEC DSM
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeendesha mafunzo kwa
wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa
kufanyika kuanzia Novemba 10 katika
halmashauri 16 nchini.
Akifungua Warsha
hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga amesisitiza kuwa
suala la nidhamu,uaminifu ,kujituma na kuzingatia taratibu kuwa silaha muhimu
katika ufanikishaji wa utekelezaji wa
mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao
umeanza kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Bw. Mwamanga ametoa msisitizo huo wakati akifungua warsha ya
siku moja ya mafunzo hayo katika ukumbi wa TEC jijini Dar es Salaam ambako
amebainisha mambo muhimu yanayochangia
TASAF kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali za utekelezaji wa shughuli
zake ukiwemo utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na zilizo katika
Mazingira hatarishi ambapo amesema kuwa nguzo kuu ni uwajibikaji wa pamoja na kuzingatia
taratbu za Mpango.
No comments:
Post a Comment