Friday, November 7, 2014

MWAKILISHI MKAZI WA UNDP NCHINI ATAKA WANANCHI WA VIJIJINI WASAIDIWE KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

IMG_4025
Mratibu  wa  mradi  wa  kudhibiti  wanyama  wakali  kwa kutumia   waya  na   mitii  maalumu  inayohimili  ukame  unaofadhiliwa na UNDP  Dr. Maurus  Msuha akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) alipotembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP  wilayani Longido  mkoani  Arusha  katika  ziara  yake  ya  siku mbili mara baada ya kuwasili wilayani humo. Katikati ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu aliyeambatana na Mwakilishi huyo.
Na Mwandishi wetu,
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka  wadau   wa  mazingira   nchini  kuwasaidia  wananchi  wa  vijijini  hasa  wafugaji   kutumia   nguvu  na rasilimali  walizonazo   kukabiliana  na  athari  za  mabadiliko  ya tabia  ya  nchi  kwa  kuendelea  kuhifadhi mazingira  na  viumbe  vilivyopo  wakiwemo  wanyamapori
Bw,  Rodriguez  aliyasema  hayo  wilayani Longido  mkoani   Arusha  katika  ziara  yake  ya  siku mbili  ya  kutembelea  baadhi  ya miradi  inayofadhiliwa  na  shirika  hilo  .
Akizungumza  baada  ya  kutembelea  na  kuzindua  mradi  wa  kuwawezesha  wafugaji   wa  wilaya  ya  Longido  kupunguza  ukataji  wa  miti   kwa  ajili   ya kujenga  uzio  wa  kulinda  mifugo  yao  na  wanyama  wakali   Bw, Rodriguez, amesema  kutokana  na  uelewa mdogo  wa  mabadiliko  yanayoendelea  kutokea  wananchi  wengi  wa vijijini  wanahitaji  msaada  wa  namna  ya  kuyadhibiti.
IMG_4027
Mratibu  wa  mradi  wa  kudhibiti  wanyama  wakali  kwa kutumia waya na mitii  maalumu  inayohimili  ukame  unaofadhiliwa na UNDP  Dr. Maurus  Msuha akiendelea kutoa maelezo kwa Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez (katikati), wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya.
Aidha  alisema  kwa  sasa  wananchi  wengi  wanatumia  muda  na nguvu nyingi  kushughulikia  matokeo   ya  athari  za  mabadiliko ya tabia ya  nchi  na  maeneo  mengi  wamekuwa  wakijikuta  wanagombana  wenyewe  kwa  wenyewe  badala  ya  kutafuta  ufumbuzi  wa matatizo  ya msingi.
"mara nyingi  wananchi wa  vijijini  kama  hawa   wafugaji  mmekuwa  wamekuwa  wakilaumiwa  kwa  matokeo ya  yale wanayoyafanya    kwa  kusukumwa  na  mabadiliko   haya   na mengine wangeweza  kuyajua  wala  wasingeyafanya "alisema  Rodriguez.
Aidha  Bw. Rodriguez  ambaye  pia ni  Mkuu  wa  miradi  ya  maendeleo  inayofadhiliwa  na  shirika  hilo  hapa  nchini  amewataka  viongozi  na  watendaji  wakiwemo  watalaam  kutumia muda   na  uwezo  wao  kuwasaidia  wananchi   wa  vijijini hasa  wafugaji  na  kwamba UNDP  itaongeza  nguvu  kusaidia  makundi hayo.
IMG_4033
 Mratibu  wa  mradi  wa  kudhibiti  wanyama  wakali  kwa kutumia waya na mitii  maalumu  inayohimili  ukame  unaofadhiliwa na UNDP  Dr. Maurus  Msuha akimwoonyesha eneo maalum lililowekwa uzio kwa ajili ya kulinda mifugo na wanyama wa kali Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez aliyefika wilani hapo kukagua miradi hiyo.
Mratibu  wa  mradi  wa  kudhibiti  wanyama  wakali  kwa kutumia   waya  na   mitii  maalumu  inayohimili  ukame  unaofadhiliwa  na UNDP  Dr. Maurus  Msuha   ambaye  pia  ni  mtafiti  mkuu  wa wanyama  katika  taasisi  ya  utafiti  wa  wanyamapori  TAWIRI  amesema  mradi huo  umeonyesha mafanikio  makubwa kwa  kuanza  kupunguza  uhasama  kati  ya  wafugaji  na  wanyama pori  wanaokula  mifugo yao  wakiwemo  Simba  na  Fisi.
Kwa  upande  wao  viongozi na wananchi  akiwemo Mkuu  wa  wilaya ya Longido  Bw  James  Ole Milya   wamesema  pamoja  na  changamoto  zinazowakabili  wanaendelea  kutilia  mkazo  suala  la  utunzaji  wa  mazingira  na  wanyamapori  kwani   licha  ya kuwa  ni  asili  yao  ndio  msingi  wa  maisha  yao.
IMG_4039
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya (kulia) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakati alipotembelea wilaya hiyo kukagua maendelo ya miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP. Kushoto ni 
IMG_4057
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akisalimiana na na wanawake wa kimasai mara baada ya kuwasili wilayani Longido kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
IMG_4064
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya kwa pamoja wakizundua uzio wa kuhifadhia mifugo ya jamii ya wafugaji wilayani Longido wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
IMG_4070
Muonekano wa uzio utakaotumika kuhifadhia wanyama wasidhurike na wanyama wakali mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
IMG_4111
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akitoa nasaha zake kwa jamii ya wafugaji wa wilaya ya Longido mkoani Arusha alipofanya ziara ya siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
IMG_4075
Baadhi ya wakazi wa Longido ambao shughuli zao kubwa ni ufugaji wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
IMG_4121
IMG_4077
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akivishwa zawadi ya shuka la kimasai na mmoja wa wafugaji wa wilaya hiyo.
IMG_4088
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisikiliza maelezo ya zawadi  za asali za Nyuki wadogo na wakubwa kutoka kwa jamii za wafugaji wanaofadhiliwa na shirika la UNDP wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani humo.

No comments: