|
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na
Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja
(aliyevaa suti nyeusi) akiwaongoza wanahabari kutembelea mradi
mkubwa wa maji uliopo katika chemichemi ya Mto
Karanga. |
|
Meneja ufundi wa Mamlaka ya Maji safi na
usafi wa Mazingira mjini Moshi,Mhandisi Patrick Kibasa akitoa maelezo
kwa wanahabari kuhusu ujenzi wa kituo cha kutibu maji katika chanzo
cha maji cha Mto Karanga. |
|
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi
wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonesha
wanahabari chanzo cha maji kilichopo Mto Karanga
. |
|
Wanahabri wakipita juu ya Bomba zilizoanza
kusambazwa kutoka katika chanzo cha maji cha Mto
Karanga. |
|
Bomba za kupitisha maji kutoka katika
Chemichemi kando ya Mto Karanga zikiwa tayari zimesambazwa kwa eneo
kubwa kwa ajili ya kupitisha maji kuelekea maeneo ya Pasua na
kwingineko. |
|
Moja ya kiungio cha bomba za maji za nchi 10
kwenda nchi 8 zilizosambazwa toka chanzo cha Chemi chemi ya Maji kando
ya mto karanga |
|
Sehemu ya kutolewa hewa katika maungio ya
bomba za maji zinazosambazwa kutoka chanzo cha maji cha Mto
Karanga. |
|
Bomba la maji likiwa limepita kando ya Mto
Karanga. |
|
Maeneo mengine mafundi walilazimika kuchimba
eneo kubwa ili mradi kwepa vipando katika maeneo ambayo Bomba hilo
limepita. |
|
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi katika
maeneo ambayo bomba hilo limepita. |
|
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na usafi wa
mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha eneo
ambalo bomba zinazosambazwa kutoka chanzo cha Mto Karanga
zitaunganishwa kwa ajili ya kupeleka maji kwa watumiaji.Eneo hilo liko
jirani na kiwanda cha Bia cha Serengeti. |
Na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.
TATIZO la
upungufu wa maji katika Manispaa ya Moshi linaelekea kuwa historia ifikapo
mwezi Desemba mwaka huu kufuatia kukamilika kwa utekelezaji wa mradi
mkubwa wa maji uliopo katika chemchem ya Mto Karanga ambao umegharimu kiasi cha
shilingi milioni 382.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ( MUWSA), Mhandisi Cyprian
Luhemeja amefafanua kuwa, mradi huo utakapokamilika utahudumia maeneo ya
Bomambuzi, Pasua , Matindigani na meneo ya katikati ya mji.
Mhandisi
Luhemeja amesema maeneo hayo kwa sasa yana mgawo wa maji kutokana na uwepo wa
maji kidogo ambapo pindi mradi huo utakapokamilika utawezesha kwa kiasi kikubwa
upatikanaji wa maji katika maeneo hayo kwa saa 24.
Amesema
mradi huo utasaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kwa mita za
ujazo zipatazo 2,592 kwa siku katika mfumo wa kusambazia maji ambapo kwa sasa
umeshakamilika kwa asilimia 99.
Amefafanua
kuwa gharama za mradi huo ni kubwa lakini gharama za uendeshaji ni ndogo
kutokana na chanzo cha maji hayo kutoka katika chemchem ya mto karanga ambapo
itasaidia upatikanaji wa maji saa 24.
No comments:
Post a Comment