Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kuzindua Kituo cha Michezo cha Kidongo Chekundu.
Na Francis Dande
MKURUGENZI
wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama amempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jakaya Kikwete kuzindua Kituo cha Kisasa cha Mafunzo ya michezo eneo la wazi la
Kidongo Chekundu, Kariakoo, jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua ujenzi wa Kituo hicho uliofanyika leo, Msama alisema Kituo hicho kitasaidia kuzalisha vijana wengi wenye vipaji
na kuandaliwa vizuri.
Hicho
ni Kituo kinachojengwa kwa udhamini wa kampuni ya Symbion ikishirikiana na
Klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa lengo la
kuinua kiwango cha sekta hiyo kitaifa na kimataifa.
Msama
ambaye ni mdau wa tasnia ya burudani kupitia uratibu wa matamasha ya muziki wa
injili ya Pasaka na Krismas, alisema kituo hicho kitakuwa mwanzo mpya wa
kuimarika kwa sekta hiyo.
Alisema,
akiwa mdau wa maendeleo ya vipaji vya aina mbambali, anaiona fursa zilizopo
kupitia kituo hicho ambacho baada ya kukamilika, kitasaidia vijana wenye vipaji
kufikia malengo kwa maslahi yao
binafsi na michezo.
Msama
alisema kwa upande wa soka, anaamini kituo hicho kilichozinduliwa
na Rais
Kikwete, kitakuwa chachu ya vipaji ambavyo nitakuwa msaada kwa timu nyingi
nchini na hatimaye timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars.
“Nampongeza
Rais Kikwete kuzindua Kituo hiki ambacho naamini kitasaidia maendeleo ya
michezo nchini kwa kuibua na kukuza
vipaji vya vijana ambao watakuwa msaada mkubwa kwa taifa,” alisema Msama.
Alisema
watanzania wana kila sababu ya kumpongeza Rais Kikwete ambaye ataondoka
madarakani mwakani baada ya miaka yake 10 ya uwepo wake madarakani akiwaachia Kituo hicho ambacho
kitabaki kama alama yake.
“Ujenzi
wa kituo hiki kilichozinduliwa na Rais Kikwete, ni habari njema kwa wadau wa
michezo na burudani, kunafungua fursa kwa vipaji vipya kuibuliwa na kuendelezwa
kwa maslahi yao na taifa,” alisema
Msama.
Alisema
japo kituo hicho kinajengwa kwa malengo ya kuibua na kuendeleza vipaji vya
michezo, anaamini kama kitakuwa na uwanja wa kutosha, hata wao Msama Promotions
ambao ni wadau wa matamasha ya injili, watapata fursa ya kuendesha matukio yao.
Msama
Promotions, ndio waasisi wa matukio ya muziki wa injili kupitia matamasha ya
Pasaka na Krismas ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki huo wa
kuutangaza ukuu wa Mungu tangu mwaka 2000.
Matukio
hayo mawili yamekuwa chachu ya kukua kwa muziki wa injili kwani yamekuwa
yakishirikisha waimbaji mahuiri wa ndani na nje ya nchi ikiwemo kutoka Kenya, Zambia,
Afrika Kusini, Rwanda
na Burundi.
No comments:
Post a Comment