Thursday, November 6, 2014

KONGAMANO LA MASWALA YA TEHAMA AFRIKA LA TAZAMIA MASWALA YA USALAMA MITANDAO

Baada ya Mwezi Oktoba kuisha ambapo kubwa lilikua ni kukuza uelewa juu ya matumizi salama ya mitandao, Taarifa ya kumalizika kwa mwezi huo inaweza kusomeka"HAPA" Mambo mengi tuliyo yajadili yameonekana kuangaziwa tena kwenye kongamano la maswala ya TEHAMA Jijini Cairo Nchini Misri. Muundo wa kongamano hili ulihusisha meza kuu inayo fungua mijadala na wasikilizaji kuchangia na kuuliza mwaswali pamoja na kupata njia ya kufikia malengo kupitia mada tofauti tofauti.

Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, Katika Meza kuu ya Mjadala alio husisshwa alipata kuzungumzia jinsi teknolojia ya habari na mawasiliano inavyo patiwa kipaumbele cha mwishoni na idara za fedha katika mataifa mbali mbali ingawa ni sekta ambayo ina nafasi kubwa sana katika kuleta mabadiliko na kukuza kwa haraka uchumi wan chi yeyote kama itatumika vizuri.

Aidha, Kwenye Meza kuu ambayo Nilikua nimehusika tulipata kuangazia maswala mbali mbali na huku nikizungumzia kwa kina jinsi usalama mitandao utakapo achwa kupewa kipaumbele unavyo weza kurudisha nyuma jitihada za dhati za kutumika vizuri kwa teknolojia ya Habari ili kukuza uchumi wan chi mbali mbali.

Pia nilipata kuzungumzia umuhimu mkubwa wa kuhakikisha mataifa ya Afrika yanaongeza jitihada ili kuhakiki Mafunzo yahusuyo usalama mitandao yanakuzwa kwa kasi ili kuhakiika wataalam wa kutosha wanapatikana na kusababisha watumiao vibaya teknolojia ya habari na mawasiliano wanaweza kuangazwa kiurahisi na kudhibitiwa kwa manufaa ya kukuza uchumi wan chi yoyote duniani.

Katika Mkutano Huu ambao Pia ulihudhuriwa na Mkuu wa  Intel  bwana John E. Davies, Kama anavyo onekana kwenye picha akiwa na Mkuu wa Intel katika Nchi ya Misri, Sikusita kukutana nao na kujadili maswala mbali mbali yahusuyo usalama mitandao huku nikitaka kujua jinsi gani Intel inajipanga kuhakiki uinzi mtandao unakua na nafasi nzuri.


Katika Kunipatia Majiibu, Nilifarijika kujua ya kua Intel imejipanga kuweka ulinzi mtandao katika vifaa vyake ambavyo kwa kushirikiana na program za Anti-virus kwa pamoja zitaimarisha ulinzi wa kina katika Komputa. Alinihakikishia hatua yao hiyo haita punguza soko la matumizi ya Anti-virus bali kwa pamoja patapatiwa namna ya kuongeza nguvu ili kukabiliana na wimbi la virusi vinavyo tumwa kwenye Komputa za watumiaji ili kuleta athar.

Aidha, Kwa Upande wa Waziri mwenye dhamana ya Sayansi na Teknolojia Nchini Misri, Enginia Atef Helmy mbali na kuonyewha kufurahi sana kuona mimi nilifanikisha kuhudhuria mkutano huo alinieleza anajitihada za dhati kuhakikisha panapatikana daraja madhubuti la kuunganisha Afrika kuanzia kusini hadi kazkazini.

Aliifafanua na kusema kwa kushirikiana Nchi za Afrika katika maswala ya Tehama na pia kuimarisha nguvu ya pamoja anaimani kabisa teknolojia ya Habari na mawasiliano ina nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko katika dunia ya kesho. Pia alinieleza kwa kina ya kua vijana ndio hasa nguvu kazi inayo itajika na dunia ya leo ili kuhakiki mambo yanasogea vizuri.

Mbali na mijadala mbali mbali, Pia palikua na matukio yakutia saini makubaliano ya kukuza ushirikiano nanchi za bara Asia pamoja na mataifa mengine. Palipatikana Ziara maalum ya kutembelea idara maalum inayo husika na maswala ya ulinzi wa mitandao wan hi ya Misri. Pale tulipata kujionea shughuli mbali mbali zinazocfanyika kuhakiki Nchi ya Misri inabaki salama mitandaoni.

Huko mbali na kujionea mengi na matumizi makubwa ya teknolojia yanavyo tumika kuhakiki Nchi inabaki salama kiimtandao. Tulipata kuonyeshwa changamoto mbali mbali walizo kumbana nazo kama taifa na ukanda mzima wa Nchi za mashariki ya kati.


Aidha, Ufafanuzi mzuri wa namna changamoto zimetumika vizuri kuwa Fursa na kuhakiki mambo yanasogea tulipata kujizwa. Na pia tulipata kuonyeshwa jia mbali mbali zinazo tumika nan chi hiyo ili kuhakiki wataalam wa maswala ya usalama mtandao wana zalishwa ipasavyo ili kuweza kukabiliana na changgamoto za uhalifu mtandao zinazo endelea kukua kwa kasi. Mengi yalikuua yanafanana na nilicho kizungumza na kituo cha "MLIMANI TV" ili kutolea ufafanuzi baadhi yam ambo.

No comments: