Monday, November 3, 2014

KINYWAJI CHA SHUDA COCKTAILS CHAZINDULIWA JIJINI DAR

Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD mwishoni mwa wiki ilizindua kinywaji cha Shuda Cocktails hafla iliyofanyika Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kinywaji hicho kimetengenezwa kwa ufanisi na kuchanganywa katika vipimo maalum ili kupata bidhaa zenye ladha nzuri zinazolenga na kukubalika na matabaka yote ya wanywaji au watuamiaji wa vileo. Ujazo wake ni 700ml. Bidhaa hii inazalishwa nchini Uingereza.

Meneja Masoko ya Kinywaji cha Shuda Cocktails, Bernadetha Daudi akiongea katika uzinduzi wa kinywaji huo mwishoni mwa wiki iliyopita Nobemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD ambao ni wasambazaji wa kinywaji cha Shuda Cocktails akiongea katika uzinduzi wa kinywaji hicho, halfa iliyofanyika  mwishoni mwa wiki iliyopita Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Shuda Cocktails zipo katika ladha nne kwa sasa: Woo Woo, Pina Colada, Mojito na On the Beach. bei ya rejareja ni Tsh 12,000 kwa chupa.
Mabinti waliokipamba kinywaji cha Shuda Cocktails.
Balozi wa Kinywaji hicho, Lemtuz akiwa na mabinti wakikipamba kinywaji cha Shuda Cocktails.
Kwa sasa zinapatikana katika supermarket zote hapa Dar es salaam, kumbi za starehe na bar kwenye kila kiunga cha Dar es salaam. Hivi karibuni, Shuda Cocktails zitapatikana mikoani pia.
Furaha ya kinywaji cha Shuda Cocktails.
Marafiki walipokutana pamoja.
Wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kinywaji cha Shuda Cocktails.
Wengine waliamua kuweka kumbukumbu.
Bongo movie nao walikuwepo.
Ukodak ulihusika toka #KajunasonStudio ya Kajunason Blog.
Mtaalam King Maluu akionyesha umahili wake wa kuitandika mdomo wa bata.
Kila mmoja alitaka kupiga picha na Msanii Diamond Platinumz.
Haya mimi pia Mmiliki wa Kajunason Blog niliweza kupata ukodak na Msanii Diamond.
Warembo nao walikuwepo kushuhudia uzinduzi huo.
Khadija Mwanamboka na Shamim Mwasha nao waliwakilisha.
Warembo wakifurahia ukodak toka #KajunasonStudio ya Kajunason Blog. Picha zote na Cathbert wa Kajunason Blog.

No comments: