Sunday, November 2, 2014

IGP MSTAAFU PHILEMON MGAYA ASHEREHEKEA MIAKA 85 YA KUZALIWA

WAZIRI Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba Watanzania  kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi zao wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania.
Msuya aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemon Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya Protea , Court Yard jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote.
“Huyu ndiye Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa. Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza.
Alisema kuwa Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na kipindi chake cha uongozi  alikuwa akitoa amri zinatekelezwa mara moja.
Naye Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono  jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda.
Aliwasihi wadau kutoa ushirikiano kwa  kampuni yake inayosambaza bia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.
                                       
“Tunatafuta maeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini. Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dkt. Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.
Wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Dkt. Fenella Mukangara, Katibu Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Anthony Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi, Mzee James Rugemalira na wengineo.
 Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa  kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)  Mzee Philemon Mgaya
Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada
 Mkuu  wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
 Keki
Waziri  Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa David Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya
 Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Mzee Philemon Mgaya
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu
 Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira akitoa pongezi zake kwa IGP Mstaafu na kuelezea  Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Mabibo Beer and Wines Mama  Benedicta Rugemalira akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu

Mshereheshaji Joe Mgaya ambaye ni Mtoto wa IGP Mstaafu Philemon Mgaya akisherehesha

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dkt. Alex Malasusa akimpongeza Mzee Mgaya
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.  Fenella Mukangara  akimpa mkono wa Pongezi IGP mstaafu


Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dkt. Alex Malasusa na Mzee Mgaya wakiwa katika Furaha
IGP Mstaafu akipokea zawadi

IGP Mstaafu Philemoni Mgaya akikata keki huku amezungukwa na wajukuu wake



Mzee Mgaya akipongezwa na Mzee James Rugemalira
Haya wajukuu na tule keki sasa....
Balozi Juma Mwapachu na Mwenyekiti Mstaafu wa Gymkhana Club Mzee George Kritsos wakipozi na Mzee Mgaya
Mzee Mgaya akipozi na baadhi ya watu mashuhuri waliohudhuria sherehe hizo
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya akiwa na mabinti wa Mzee Msangi











 Watu mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo




 Burudani ya nguvu

No comments: