Rais
wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akipongezana na
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto) baada
ya kuzindua kadi maalum za Safari za kampuni hiyo zitakazomwezesha
dereva kupata huduma ya mafuta kutoka vituo vyote vya Gapco nchini kwa
unafuu. Wengine (kustoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai,
Ashok Dhar, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara, Ofisa Mtendaji
Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na Mkurugenzi
wa kituo cha Gapco, Barabara ya Nyerere, Muntazir Bharwani.
Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akikabidhi
kadi maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara na
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki baada ya kuzindua kadi
hizo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika
hafla iliyofanyika Kituo cha Mafuta Gapco cha Kamata, Dar es Salaam
jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai,
Ashok Dhar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk.
Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Rais
wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok akionesha kadi maalum
za Safari za Gapco baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika
kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Kadi hizo
zitamwezesha dereva kuweza kupata huduma ya mafuta kwa unafuu kutoka
vityo vyote vya Gapco Tanzania. Kutoka kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu
wa Gapco Tanzania, Vijay Nair, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum
Bisarara, Diwani wa Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto),
Meneja Miradi wa Gapco, Mohit Shirma, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la
makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Meneja
Uendeshaji wa Kadi za Gapco, Shital More akielezea matumizi ya kadi
maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki
(katikati) baada ya kuzindua rasmi kadi hizo zitakazomwezesha dereva
kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika vituo vyote vya Gapco nchini
katika hafla iliyofanyika kituo cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana.
Wengine (kutoka kushoto) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya
Gapco, Dk. Macharia Irungu, Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit
Shirma, Rais wa kampuni ya Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok
Dhar na maofisa wengine wa Gapco.
Diwani
wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa pili kulia) akifurahia
jambo baada ya kuelekezwa matumizi ya kadi maalum za Safari Gapco na
Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit Shirma baada ya kuzindua kadi
hizo, katika kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana.
Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk.
Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu
akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi
maalum za Safari zitakazomuwezesha dereva kupata unafuu wa mafuta kutoka
katika vituo vyote vya Gapco, Dar es Salaam jana.
Diwani
wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki akizungumza na wageni waalikwa
wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi maalum za Safari zitakazomuwezesha
dereva kupata unafuu wa mafuta kutoka katika vituo vyote vya Gapco, Dar
es Salaam jana.
---
Kampuni
inayoongoza kwa uuzaji wa bidhaa za mafuta nchini, imezindua programu
aminifu kuwezesha wamiliki wa magari kujipatia pointi wakinunua mafuta
ambazo zitawawezesha kupata ‘Mafuta Bure’ Kama faida.
Mpango huu utawanufaisha wakazi wa Dar es Salaam, kwa kuanzia na nchini kote mwakani.
Jerry
Slaa, Maya wa Manispaa ya Ilala akizungumza katika sherehe ya uzinduzi
iliyofanyika katika kituo cha GAPCO Kamata jijini Dar es Salaam alisema:
"kuanzishwa kwa programu ya GAPCO Safari kutasaidia kutatua changamoto
za muda mrefu zinazowakabili wamiliki wa magari nchini. Mfumo huu ni
muhimu kuelekea jamii ya kufanya malipo bila fedha taslimu.”
Slaa
alipongeza GAPCO kwa kuwa Kampuni ya kwanza katika sekta ya mafuta
Kurudisha thamani ya fedha kwa wateja wake nakuomba Kampuni zingine
kufuata nyayo za GAPCO.Alibainisha kuwa huduma hii itasaidia kupunguza
kwa ujumla, gharama za mafuta, kupunguza bugudha ya makaratasi na
kusaidia kuendesha biashara kwa ufanisi zaidi.
Slaa
aliongeza kwamba maendeleo kama hayo ni muhimu katika kuboresha uchumi
wa nchi kwa kuwa usafiri ni moja ya nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania.
Slaa alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ili
kuboresha sekta ya usafiri nchini.Dr Macharia Irungu, Afisa Mtendaji
Mkuu (CEO) GAPCO Group alisema GAPCO ina maslahi mapana katika soko la
Afrika Mashariki na inajivunia kuwa na vituo vya mafuta 63 nchi nzima,
na kuifanya GAPCO kuwa moja ya kampuni ya mafuta inayoongoza.
Akimkaribisha
Mgeni Rasmi kuzindua rasmi mpango, Bw. Ashok Dhar, Rais wa Reliance
Industries Limited India, kampuni mama ya GAPCO Tanzania Ltd, alisema
kuwa mpango huu unawakilisha sehemu ndogo ya faida ya GAPCO.Bw. Dhar
alisema anaimani na Uchumi wa Tanzania, na hivyo kampuni yake itaendelea
kuwekeza zaidi nchini kwa miaka ijayo.
Akifafanua
zaidi juu ya programu ya GAPCO Safari, Vijay Nair, Afisa Uendeshaji
(COO) alisema kuwa kadi za Gapco Safari zitakuwa zinapatikana wakati
wowote katika vituo vya mafuta vya GAPCO mkoani Dar Es Salaam kwa
kuanzia.mtendaji alieleza kuwa huduma hiyo ilikuwa wazi kwa wamiliki
binafsi, kampuni na wafanya biashara ya magari.
"Tunataka
kuboresha zaidi huduma zetu za uuzaji mafuta kwa wateja wetu. GAPCO
tunaandhisha huduma ya kutoa huduma aminifu ambayo ni suluhisho kwa
wamiliki wa magari nchini kote… Hii ni huduma ya kipekee tuliyo ianzisha
tukiamini kupitia Kauli mbiu ‘……….’," alisema Bw Nair.
No comments:
Post a Comment