Doris Mollel akikabidhiwa vitabu 200 na mkurugenzi wa MAK Solutions Bi Meetal Kirubakaran. Vitabu hivyo vilikabidhiwa kwa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma kama mchango wa kuadhimisha siku ya watoto duniani.(Picha zote na Albert Manifester).
Dodoma, Novemba 2014.
Katika kuadhimisha siku ya watoto duniani inayofanyika tarehe 20 Novemba kila mwaka, Mrembo wa Redds Miss central Zone 2014 Doris Mollel amechangia Vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) katika shule ya msingi Mpunguzi iliyopo katika kijiji cha Mpunguzi mkoani Dodoma.
Doris, ambaye pia ni mshindi wa tatu kwenye Redds Miss Tanzania 2014 amejikita katika sekta ya elimu kama sehemu ya huduma zake za jamii ambapo amedhamiria kuendeleza mchango kwenye elimu ya msingi kwa kuchangia vitabu kwenye shule zenye uhitaji zaidi.
Msaada huo wa Vitabu 200 vya kiada na ziada ameutoa kwa ushirikiano na kampuni ya uuzaji wa Vitabu ya MAK Solutions yenye duka lake Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Meetal Kirubakaran alisema MAK solutions wanafurahi kutoa vitabu hivyo kama mchango wao katika kusaidia sekta ya elimu Tanzania.
Doris akijadiliana jambo na Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda (Katikati) mjini Dodoma kabla ya kuelekea Mpunguzi. Wa kwanza kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na anayefuata ni Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela.
Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mollel alisema ‘Ni muhimu kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea tangu wakiwa wadogo ili kuwakuza kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa ambayo inahitaji uelewa mpana. Najivunia kuwa sehemu ya kampeni hii na nitaendelea kuongeza jitihada za kuwafikia watoto wengi zaidi’
Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda amempongeza Doris kwa juhudi zake za kusadia jamii hasa sekta ya elimu na ameomba wadau wengi kuiga mfano huu kuendeleza sekta hii.
Hafla hiyo ya makabidhiano ilihuduriwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mpunguzi Bi Neema Mando, Makamu mwalimu mkuu wa shule Bw Danctan Chipalo, Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo, Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela pamoja na wanafunzi wote wa shule ya Mpunguzi.
Alipokuwa njiani kuelekea mpunguzi, Doris alipata nafasi ya kuongea machache na baadhi ya wanafunzi wa vijiji vya jirani.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini.
Doris Mollel (kulia) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili shuleni Mpunguzi. Kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya mpunguzi Bi Neema Mando.
Doris akiuleza uongozi wa shule nia na madhumi ya safari yake. Kushoto ni mwalimu mkuu msaidizi Bw Danctan Chipalo na mwalimu mkuu Bi Neema mando.
Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo akimsaidia Doris kuchambua vitabu hivyo kutoka kwenye boksi la MAK Solutions Ltd.
Doris akiwaeleza wanafunzi umuhimu wa kupenda kujisomea tangu wakiwa wadogo.
Kutoka kushoto: Bw Danctan Chipalo, Bw Mnyagatwa Mazengo Bi Neema Mando na Doris.
Doris akiwa na baadhi ya wanafunzi baada ya kugawa vitabu.
Wanafunzi wakifurahia vitabu vyao.
Akimuelekeza mmoja wa wafunzi juu ya mambo yaliyomo kwenye kitabu cha ‘WATER’
Wakiwa na Vitabu.
Makabidhiano.
Doris akiongea jambo na mwalimu mkuu mara baada ya makabidhiano hayo.
Akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye viwanja vya shule hiyo muda mfupi kabla ya kuondoka shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment