Sunday, October 5, 2014

WASHINDI WA MBIO ZA BAISKELI ZA SHIMIWI WATUNUKIWA MEDALI

 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya dhahabu mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka  Hazina, Prisca Kahimba (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake kutoka RAS Pwani akijitahidi kukaza mwendo katika mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI  mjini Morogoro leo.
 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya fedha mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka  RAS Pwani, Agatha Gambi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake kutoka Uchukuzi Johari Moshi akimalizia mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI  mjini Morogoro leo.
 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka  Uchukuzi, Johari Moshi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanaume za SHIMIWI kutoka Ikulu John Fataki akiwasili kituo cha mwisho cha mbio hizo cha Lake Oil kutoka kituo cha njia panda ya Mkata mjini Morogoro leo.Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya dhahabu mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka  Utumishi, Hassan Ligoneko (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanaume za SHIMIWI kutoka Utumishi Hassan Ligoneko akiwasili kituo cha mwisho cha mbio hizo cha Lake Oil kutoka kituo cha njia panda ya Mkata mjini Morogoro leo.
 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya fedha mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka  RAS Tanga, Ezekiel Mhina (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka  RAS Tanga, Ezekiel Mhina
 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka  Ikulu, John Fataki (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
 Polisi wa usalama barabarani akizuia magari kabla ya kuanza kwa mbio za baiskeli za wanawake za kilomita 32 katika mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro.
 Washiriki wa mbio za baiskeli za wanawake za kilomita 32 za SHIMIWI, wakianza mashindano katika kituo cha Melela Mlandizi mjini Morogoro leo.
 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake za kilomita 32 kutoka Uchukuzi Johari Moshi (kulia) akijaribu kuwapita washiriki wenzake katika mashindano ya mbio za baiskeli ya SHIMIWI  mjini Morogoro leo.
 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake wa RAS Pwani Agatha Gambi akiwa amewaacha washiriki wenzake umbali mrefu baada ya kuanza kwa mashindano ya mbio za baiskeli ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.
 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake za kilomita 32 kutoka Hazina Prisca Kahimba akikazana baada ya kumpita mshiriki wa RAS Pwani (hayupo pichani) katika mashindano ya mbio za baiskeli ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.
 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake wa Hazina Prisca Kahimba akikata mbuga
 Baadhi ya watumishi wa Serikali kutoka Wizara,Idara Zinazojitegemea na Wakala wa Serikali wakisubiri msafara wa mbio za baiskeli za wanawake kuwasili katika kituo cha Lake Oil mjini Morogoro leo.
 Watumishi wa Hazina wakishangilia baada ya mchezaji wao kuwasili kituo cha mwisho cha mbio za baiskeli cha Lake Oil mjini Morogoro leo.
 Furaha ya wana Hazina haina kikomo
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake wa Hazina Prisca Kahimba akimalizia mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI  mjini Morogoro leo. Picha zote na Happy Shayo

No comments: