Kampuni maarufu ya kuuza muziki kwa njia ya digitali inayojulikana kama Deezer, imeingia ushirikiano na kampuni ya Vodacom ambapo wateja wa Vodacom wataweza kupakua muziki katika maktaba kubwa ya muziki ya kampuni hiyo yenye nyimbo zaidi ya milioni 35.
Deezer ni kampuni kubwa ya kuuza muziki kwa njia ya kidigitali nchini Afrika ya kusini.Katika kusherehekea ushirikiano huu na Vodacom wateja wapatao 17 milioni wa Vodacom watajipatia offer ya kipindi cha mwezi mmoja ya kupakua bure muziki wa aina mbalimbali kutoka maktaba kubwa ya muziki ya kampuni ya Deezer.
“Kupitia ushirikiano huu wateja na wapenzi wamuziki nchini Afrika ya Kusini wataweza kupata muziki kutoka sehemu mbalimbali duniani na uzuri wa huduma hii ya kiteknolojia ni rahisi kinachotakiwa ni kujisajili na kuanza kupakua muziki uupendao kutoka maktaba kubwa ya muziki wa kidijitali ya Deezer”Anasema Phil Patel,Mtendaji Mkuu wa Uendelezaji wa Biashara wa Vodacom.
Kufaidi huduma hii anachopaswa kufanya mteja wa Vodacom popote alipo ni kujisajili kwa kutembelea tovuti ya http://live.vodafone.com/deezer.Baada ya kujisajili itakuwa rahisi kuanza kupakua muziki aupendao,offer ya mwezi mmoja ya kupakua muziki bure imeanza oktoba 9 mwaka huu.
“Hii ni hatua kubwa kikampuni kuweza kutoa offer ya mamilioni ya wateja kupakua muziki kila mtu aupendao bure nchini Afrika ya Kusini na nchi nyinginezo.Tunaamini wateja wetu wakishajaribu huduma ya kupakua muziki wakidigitali kutoka Deezer hawatarudi nyuma”Anasema Patel.
Anaongeza kwamba muda wa offer ukiisha wateja wa Vodacom Afrika ya Kusini watatakiwa kulipia huduma hii Randi 59.99 kwa mwezi au wasiotaka kuendelea kupata huduma hii watajitoa.Watakaoendelea kupata huduma hii watatozwa malipo yao kupitia akaunti zao za Vodacom na wale wanaotumia huduma ya malipo ya kablla watalipa gharama hizi kwa njia ya kununua muda wa maongezi.
“Kwa gharama ndogo isiyofikia kununua CD moja ya muziki kwa mwezi,unaweza kupakua miziki ya wasanii mbalimbali duniani wakati wowote upendao na uzuri muziki wa Deezer uko katika viwango vya juu na ukishapakua nyimbo zako unaweza kuzisikiliza wakati wowote na popote hata bil kujiunganisha na mtandao wa internet.Huduma hii inaleta mapinduzi makubwa katika Nyanja ya muziki duniani na Afrika ya kusini na naamini kila mtu atafurahia huduma hii ya kupata muziki kwa njia ya kidigitali”.Anasema Patel.
Naye Afisa Undelezaji wa Biashara wa Deezer Clément Cezard, amesema kampuni yake imefurahi kushirikiana na kampuni kubwa ya Vodacom katika kukuza masoko ya muziki na anaamini wateja wa Vodacom wa Afrika ya Kusini na nchi nyinginezo watafurahia huduma hii ya kupata muziki kwa njia ya kidigitali.
No comments:
Post a Comment