Wajumbe
wa Kamati ya Watoa Maamuzi Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo
katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wa nchi zilizo katika Bonde la
Ufa wakijadiliano jambo wakati wa kikao cha wajumbe hao kujadilia
masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Jotoardhi kwa nchi wananchama.
Baadhi
wa Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wan chi zilizo katika Bonde la
Ufa wakiendelea na kikao kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa na nchi
wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao, kuangalia faida
zalke, changamoto na namna ya kuzitatua.
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo yanayoendelea leo kabla
ya kufunguliwa rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa ya Jotoardhi akitoa
mafunzo kwa baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo jijini
Arusha.
Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi
Na Asteria Muhozya, Arusha.
Tanzania
imeeleza mipango yake ya kuendeleza masuala yanayohusu nishati jadidifu
mbele ya Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa
katika kongamano la Tano la Kimtaifa la Jotoardhi linaloendelea jijjini
Arusha.
Akizungumza
mara baada ya kikao hicho kwa niaba ya Kamishna Msaidizi
anayeshughulikia masuala ya Jotoardhi Wizara ya Nishati na Madini, Bw.
Paul Kiwele amesema kuwa lengo la kukutana kwa kamati hiyo ni
kuzungumzia hatua zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya
jotoardhi katika nchi zao.
Bw.
Kiwele ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo
ameeleza kuwa, lengo jingine la kikao hicho ni kuangalia faida
zilizopatikana kupitia nishati hiyo pamoja na kuangalia changamoto
mbalimbali na kuona namna bora ya kuzitatua.
Ameongeza kuwa, pendekezo la nchi wanachama kupata misaada mbalimbali ya kuendeleza masuala ya jotoardhi katika nchi zao ikiwemo
ya kifedha limepitishwa na mashirika kadhaa ikiwemo Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhifadhi wa Mazingira ( UNEP) na Umoja wa nchi zilizo katika bonde la Ufa (ARGEO).
Aidha,
Bw, Kiwele ameongeza kuwa, kikao hicho kimeamua kuipa nafasi Tanzania
kusaidiwa kuendeleza masuala ya jotoardhi katika eneo lenye viashiria
vya jotoardhi la Ngozi, Mkoani Mbeya.
Kikao
hicho cha Kamati ya Watoa Maamuzi ni miongoni mwa shughuli
zinazoendelea katika kongamano la tano la jotoardhi ambapo linakwenda
sambamba na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kuhusu masuala ya jotoardhi
ikiwemo masuala ya utafiti, uchorongaji na masuala ya fedha.
Kongamano
hilo litafunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal jijini
Arusha na litawashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali
duniani.
No comments:
Post a Comment