
Jumla ya wachezaji 26 wa Timu ya Stand United waliotua Mjini Bukoba Jana kwa ajili ya Kipute cha Ligi kuu Vodacom msimu wa 2014-15 na Wenyeji wao Kagera Sugar wamefanya mazoezi yao kwa mara ya kwanza Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba.Wachezaji hao 26 wakiongozwa na Kocha Mkuu Emmanuel Massawe pamoja na Viongozi wengine 6. Timu ya Stand United ya Shinyanga ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda Ligi na kesho Jumamosi inataka Kuibana Timu ya Kagera Sugar ambao ndio wenyeji wao ambao pia wanashikilia nafasi ya sita kwenye Ligi hiyo ya Vodacom kwa msimu huu ulioanza hivi karibuni. Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Kagera wanaingia wakiwa nafasi ya nne na pointi zao 4 huku Stand United wakiwa nafasi ya 8 nao wakiwa wanalingana pointi na Kagaera Sugar.










No comments:
Post a Comment