Ikiwa ni muendelezo
wa Semina za Fursa zinazoendelea katika mikoa mbalimbali, licha ya kuwa ni
siku ya Sikukuu ya Idd El Hajj tarehe 05/10/2014, Semina ya Fursa yashamiri mjini
Dodoma na kuvutia umati mkubwa wa watu.
Umati huo ulivutiwa
sana na huduma na mafao yatolewayo na NSSF kama vile Matibabu bure kwa
mwanachama na wategemezi wake na mikopo kupitia Saccos.
NSSF iliwasihi watu
wajiunge na mfuko huu ili waweze jipatia Fursa za kuboresha maisha yao.
Semina ya Fursa
Dodoma ilirushwa Live na kituo cha Redio cha Clouds FM katika mkoa wa
Dodoma na hivyo kuwapa Fursa hata wale
walioshindwa kufika ukumbini kusikia mada zilizotolewa popote walipo ndani ya
mkoa wa Dodoma.
Semina hizi za NSSF Fursa chini ya usimamizi wa Clouds Media zimefanyika katka mikoa ya Geita, Songea, Morogoro, Mbeya, Singida na Dodoma.
Semina hizi zonaendelea ili kuwapa FURSA Watanzania wa mikoa mingine 6 ya Mtwara, Mwanza, Kagera, Arusha, Moshi na Dar es Salam kujiandikisha na NSSF na kujipatia mafao mbalimbali.
Mkurugenzi wa
Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
akitoa mada katika Semina ya Fursa Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa kwanza kulia), Meneja wa NSSF
Mkoa wa Dodoma, Kirondera Nyabuyenze (wa pili kulia) na Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba (wa tatu kulia) wakiwa katika semina ya Fursa
Dodoma.
Mkuu wa Idara ya
Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume (wa tatu kushoto) na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Kirondera Nyabuyenze (wa pili kushoto) wakifutilia kwa
makini mada iliyokuwa ikitolewa katika semina ya Fursa Dodoma.
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa mada katika Semina ya Fursa
Dodoma.
Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa watu waliohudhuria semina hiyo.
Mwanamuziki wa kizazi
kipya Mwasiti Almasi akiwahamasisha wananchi waliohudhuria semina hiyo
wajiunge na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili waweze jipatia Fursa
za kuboresha maisha yao ya sasa na ya baadae. Kushoto ni Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba.
Maofisa wa NSSF, Gabriel Nkakatisi (kushoto) na Anna Nguzo
wakiandikisha wanachama wapya baada ya kumalizika kwa semina ya Fursa
iliyofanyika siku ya sikukuu ya Idd El Hajj mjini Dodoma.
Baadhi ya watu wakijiandikisha
katika banda la NSSF baada ya semina ya Fursa
Dodoma.
No comments:
Post a Comment