Ikiwa ni muendelezo
wa Semina za Fursa zinazoendelea katika mikoa mbalimbali, licha ya kuwa ni Siku ya Sikukuu ya Idd El Hajj tarehe 05/10/2014, Fursa Semina yashamiri mjini Dodoma
na kuvutia umati mkubwa wa watu.
Umati huo ulivutiwa na huduma na mafao yatolewayo na NSSF kama vile Matibabu Bure kwa
mwanachama na wategemezi wake, mikopo kupitia Saccos, Mafao ya kuumia kazini,
Pensheni ya Uzeeni, Pensheni ya Urithi, Msaada wa Mazishi na Pensheni ya
Ulemavu.
NSSF iliwasihi watu
wajiunge na mfuko huo ili waweze jipatia Fursa za kuboresha maisha yao ya sasa
na ya baadae.
Semina ya Fursa
Dodoma ilirushwa Live na kituo cha Redio cha Clouds FM katika mkoa wa
Dodoma na hivyo kuwapa Fursa hata wale
walioshindwa kufika ukumbini kufuatilia mada mbalimbali zilizotolewa popote walipo ndani ya mkoa huo.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa kwanza kulia), Meneja wa NSSF
Mkoa wa Dodoma, Kirondera Nyabuyenze (wa pili kulia) na Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba (wa tatu kulia) wakiwa katika semina ya Fursa
Dodoma.
Mkuu wa Idara ya
Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume (wa tatu kushoto) na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Kirondera Nyabuyenze (wa pili kushoto) wakifutilia kwa
makini mada iliyokuwa ikitolewa katika semina ya Fursa Dodoma.
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa mada katika Semina ya Fursa
Dodoma.
Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa watu waliohudhuria semina hiyo.
Mwanamuziki wa kizazi
kipya Mwasiti Almasi akiwahamasisha wananchi waliohudhuria semina hiyo
wajiunge na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili waweze jipatia Fursa
za kuboresha maisha yao ya sasa na ya baadae. Kushoto ni Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba
Maofisa wa NSSF, Gabriel Nkakatisi (kushoto) na Anna Nguzo
wakiandikisha wanachama wapya baada ya kumalizika kwa semina ya Fursa
iliyofanyika siku ya sikukuu ya Idd El Hajj mjini Dodoma.
Baadhi ya watu wakijiandikisha
katika banda la NSSF baada ya semina ya Fursa
Dodoma.
No comments:
Post a Comment