Saturday, October 25, 2014

MAHAFALI KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI EDEN GARDEN EDUCATION TRUST


Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust ya Mkoani Kilimanjaro wanaotarajia kufanya mitihani yao ya mwisho siku chache zijazo wakiingia ukumbini kwa ajili ya sherehe ya kuwaaga iliyofanyika shuleni hapo,Mbele ni mkuu wa Utawala shuleni hapo Peter Nayor .
Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Eden Garden Education Trust wakiingia kwa madoido uwanjani.
Baadhi ya wazazi wenye watoto wao katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust wakifuatilia sherehe za kuaga wahitimu wa kidato cha nne.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust wakifurahia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika sherehe yao ya kuagwa.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Eden Garden Education Trust waliofika kwa ajili ya kuwaaga wenzao wa shule ya sekondari.
Mkuu wa Utawala katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust Peter Nayor(kulia)akiteta jambo na Mgeni rasmi katika mahafali hayo Clement Kwayu ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai.
Muwakilishi wa wazazi wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust Dk John Kaleshu akiteta jambo na mkuu wa shule ya Msingi ya Eden Garden Samweli Binyanya.
Wanafunzi katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust wakionesha umahiri wa kucheza muziki.
Wanafunzi wa shule ya msingi Eden Garden Education Trust wakiimba wimbo wa kuwaaga ndugu zao wa kidato cha nne.
Wanafunzi wakionesha umahiri katika kucheza Sarakasi.
Mkuu wa shule ya sekondari Eden Garden Education Trust Thomas Muthiah akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa wahitimu .
Mwenyekiti wa Bodi na Mwanzilishi wa Shule zilizoko chini ya Eden Garden Education Trust,za Chekechea,Msingi na Sekondari Bibiana Nayor akizungumza wakati wa mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne shuleni hapo.
Mkuu wa Utawala katika shule za Eden Garden Education Trust ,Peter Nayor akizungumza wakati wa mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne shuleni hapo.
Wanafunzi wa kidato cha nne Geoge Kaleshu na Yunis wakishirikiana kusoma risala maalumu kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kuwaaga yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Eden Garden Education Trust.
Mwakilishi wa wazazi wenye watoto wanao hitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Eden Gareden Education Trust  ,Dk John Kaleshu akizungumza kwa niaba ya wazazi katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi hao wanaotarajia kufanya mitihani yao ya mwisho hivi karibuni.
Mgeni rasmi katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust ,Clement Kwayu akitoa hotuba yake kwa wageni na wanafunzi waliofika katika sherehe hiyo.
Wanafunzi wa kidato cha nne wakionesha umahiri wa kucheza .
Wanafunzi wa shule ya sekondari Eden garden Education Trust wakapata fursa yakuonesha Mavazi ya aina mbalimbali.
Kisha mgeni rasmi ,Kwayu akahitimisha kwa kutoa vyeti kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: