Tuesday, October 7, 2014

KINANA ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA CHIFU MKWAWA, KALENGA, IRINGA - APEWA HESHIMA YA CHIFU WA WAHEHE

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia fuvu la aliyekuwa Chifu wa Wahehe, Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya shujaa huyo aliyepambana na wajerumani na kujiua kwa bunduki baada ya kuona yupo hatarini kukamatwa na wajerumani.
 Picha ya kuchora ya Chifu Mkwawa
 Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akimkaribisha Kinana kutembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa katika Kijiji cha Kalenga, Iringa Vijijini wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Fuvu la Chifu Mkwa likiwa limehifadhiwa katika makumbusho hayo.
 Zuberi Mwamitala akimuonesha Kinana maandishi ya kiarabu aliyowahi andika Chifu Mkwawa enzi za uhai wake
 Mwamitala akionesha kisanduku kilichokuwa kimehifadhi fuvu la Chifu Mkwawa nchini Ujerumani na hatimaye kurejeshwa nchini.
 Mwamitala ambaye ni mtunza kumbukumbu katika makumbusho ya Mkwawa, akionesha baadhi ya mabomu yaliyotumiwa na askari wa kihehe waliopambana na wajerumani
 Kinana akioneshwa madini ya chuma yaliyotumiwa enzi za Chifu Mkwawa kutengenezea silaha mbalimbali pamoja na shoka na majembe.
 Kinana akiangalia zana za kijadi zilizokuwa zinatumiwa na jeshi la Chifu Mkwawa katika mapambano dhidi ya maadui
 Kinana akiangalia bunduki aina ya gobole la kisasa lililokuwa linatumiwa na jeshi la kijadi

 Kinana akiangalia bunduki iliyotengenezwa enzi za jeshi la Chifu Mkwawa na kutumika katika vita dhidi ya Wajerumani ambapo wazawa hao walifanikiwa kuua zaidi ya askari wa kijerumani 500
 Kinana akipiaga rimba lililokuwa linapigwa na Chifu Mkwawa enzi za uhai wake
 Kinana akiangalia makuburi ya Spika wa Bunge la Tanzania, marehemu Adam Sapi Mkwawa na mkewe ambayo ni sehemu ya kumbukumbu katika makumbusho hayo
Kinana akiwa na Chifu Abdul Mkwawa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu pamoja na msaidizi wa chifu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwa katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kalenga, Iringa Vijini, walipoanza ziara ya siku sita za kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za watu na kuzitafutia ufumbuzi.Katika mkutano huo Kinana aliitaka Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuwatafutia soko la uhakika wakulima.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akivishwa vazi la kimila la wazee wa kabila la Wahehe ikiwa ni heshima kwake.
 Kinana akivishwa kilemba
 Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila baada ya kukabidhiwa mkuki.


Kinana akiwa amekaa na Chifu Abdul Mkwawa pamoja na wazee wa kimila wa kabila la wahehe.
 Kinana akipendeza na vazi la kihehe huku akiwa na mkuki mkononi.


 Kinana akihutubia katika mkutano huo huku akiwa amevalia kimila.

 Kinana akihutubia huku akiwa juu ya kichuguu alichokuwa akikitumia Chifu Mkwawa enzi hizo kuwahutubia wananchi wake.

 Kinana akishiriki kuvua samaki katika moja ya mabwawa ya umoja wa akina mama Kata ya Kalenga.


 Kinana akishiriki kupulizia dawa katika shamba la mfano la nyanya katika Kata ya Kalenga.

 Kinana akiongozana na wananchi baada ya kukagua mradi wa ufugaji samaki na shamba la nyanya katika Kata ya Kalenga
 Kinana akiwa na Balozi wa Shina la CCM namba moja Kata ya Kalenga alipombelea na kuzungumza na wanachama wa CCM
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika mkutano huo.

No comments: