Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata mlo nyumbani kwa Balozi Lucas Mtumbuka (kushoto)wa Shina namba moja eneo la Mkimbizi, alipokwenda kumtembelea yeye na wananchama wake wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Jimbo la Iringa Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akichukua mhogo ambao ni sehemu ya vyakula alivyoandaliwa na balozi
Watoto wakipanda kwenye uzio wa nyumba ili wapate kumuona Kinana alipomtembelea Balozi, Lucas Mtumbuka, eneo la Mkimbizi
Kinana akiingia kwenye ukumbi kuzungumza na wanachama 707 wa kikundi cha Iringa Masoko Vicoba ambapo aliahidi kuwasaidia kuipata mkopo mkubwa wa fedha watakazokuwa wanakopeshana.
Kinana akizungumza na madereva wa daladala baada ya kuzindua tawi la wakareketwa wa CCM, mjini Iringa leo. Tawi hilo lina wanachama 60.
Mama Lishe akimnawisha mikono Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambapo yeye na viongozi pamoja na baadhi ya wananchama wa CCM walikwenda kupata chakula cha mchana kwa mama lishe katika Soko Kuu la Iringa leo.
Kinana akiapata mlo wa mchana kwa mama lishe mjini Iringa leo wakati wa mapumziko ya ziara ya kuimarisha uhai wa chama.Kulia ni Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya Iringa Mjini, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu.
Mbunge wa Viti Maalum, Rita Kabati (kushoto) akiwa na viongozi wengine wa CCM wakipata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, mjini Iringa leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga (katikati) akiwa na viongozi wengine wa CCM wakati wa chakula cha mchana kwa mama lishe.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chongolo, akipata mlo huo wa mchana kwa mama lishe.
Wanahabari ambao baadhi yao wako kwenye msafara wa Kinana wakipata mlo wa mchana kwa mama lishe
Kinana akiondoka baada ya kupata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, katika Soko la Iringa Mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihuubia huku mkono wake ukiwa umefungwa POP, katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa, mjini Iringa leo wa kuhitimisha ziara ya siku sita mkoani Iringa ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Wananchi wakicheza kwa furaha wakati kikundi cha Bendi ya CCM, kikitumbuiza kwa wimbo wa Ilani ya Chama wakati wa mkutano huo.
kikundi cha Bendi ya CCM, kikitumbuiza kwa wimbo wa Ilani ya Chama wakati wa mkutano huo.
Ni furaha kwa kwenda mbele kadri muziki wa wimbo huo ulipokuwa unapigwa uwanjani hapo
Nape akifarijiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Amina Imbo wakati wa mkutano huo
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuelezea mipango ya chama hicho kulikomboa jimbo la Iringa linaongozwa sasa na Chadema.
Nape akishuka jukwaani baada ya kuhutubia katika viwanja vya Mwembetogwa, Iringa Mjini
Aliyewahi kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga wa Chadema kura za maoni, Sanga Abubakar akitangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Mdillah Sekomu akitangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM
Msemaji wa Bodaboda, Adam Kindole Mkoa wa Iringa, akielezea jinsi wanavyonufaika na CCM kwa biashara yao ya kubeba abiria mjini
Waendesha Bodaboda wakishangilia risala iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho cha waendesha pikipiki
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia katika mkutano huo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chngolo akimuaga Kinana Uwanja wa Nduli akirejea Dar es Salaam.
Kinana akiagana na viongozi wa CCM uwanjani hapo
Kinan akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiingia kwenye ndege, tayari kwenda Arusha na hatimaye DSM
Kinana akiagana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu
Ndege iliyombeba katibu mkuu
Viongozi wa chama na Serikali wakipungia mkono wakati ndege iliyombeba Kinana ikipaa
No comments:
Post a Comment